TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA SHINYANGA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 18/07/2017

 TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA SHINYANGA KWA  VYOMBO VYA HABARI  TAREHE  18/07/2017   YAMETOKEA MATUKIO YAFUATAYO;   
(1)  AJALI YA  TELA LA TREKTA KUPINDUKA , KUSABABISHA KIFO NA MAJERUHI.          TAREHE 17.07.2017 SAA 06. 00 KATIKA KIJIJI CHA SOLWA,KATA YA 
SOLWA,TARAFA YA NINDO,WILAYA YA  SHINYANGA (V) MKOA WA  SHINYANGA TELA YA TREKTA AINA YA MASSEY FERGUSON NO ZA USAJILI T 740 DJU LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA MTU AMBAYE HAJATAMBULIKA  LILIPINDUKA NAKUSABABISHA KIFO CHA LUCAS S/OMETHUSELA,46YRS,MKULIMA,MSHASHI,MKAAZI WA SOLWA.PIA KUSABABISHA MAJERUHI KWA NDAMO S/O CHEREHANI,38YRS,MKULIMA,MSUKUMA,MPAGANI,MKAZI WA SHIRIMA.CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. UFUATILIAJI WA KUMTIA MBARONI DEREVA HUSIKA UNAENDELEA.

(2)  AJALI YA MOTO KUUNGUZA BWENI NA KUTEKETEZA MALI. TAREHE 17.07.2017 MAJIRA YA SAA 0800 KATIKA   SHULE YA SEKONDARI YA BUNAMBIYU KIJIJI NA KATA YA BUNAMBIYU TARAFA YA MONDO WILAYA YA KISHAPU   MKOA WA SHINYANGA WILFRED S/O JOHN, 28YRS MSUKUMA, MWALIMU WA  SHULE YA SEKONDARI BUNAMBIYU ALIBAINI BWENI KUUNGUA MOTO NA KUTEKETEZA MALI  ZA WANAFUNZI WA KIKE 26  WALIOKUWA  WANALALA KATIKA BWENI HILO. THAMANI YA MALI ILIYOTEKETEA BADO HAIJAFAHAMIKA HAKUNA MADHARA KWA BINADAMU. CHANZO CHA MOTO BADO  KINACHUNGUZWA.

(3)AJALI YA NYUMBA KUUNGUA MOTO NA KUSABABISHA HASARA YA MALI. TAREHE 17.07.2017 SAA  16:00 HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MHUNZE YA JUU MJI MDOGO WA MHUNZE KATA,TARAFA, NA WILAYA YA KISHAPU MKOA WA SHINYANGA NYUMBA YA  AMANI S/O ISSA, MIAKA 39,MSUKUMA, MKULIMA, MFANYABIASHARA, MKAZI WA MHUNZE ILIUNGUA MOTO NA KUTEKETEZA MALI ZILIZOKUWEMO NDANI ZENYE THAMANI YA TSH:100,000,000/= HAKUNA MTU YEYOTE ALIYEDHURIKA  CHANZO CHA TUKIO  KINACHUNGUZWA.     
                   
 (4)   KUPATIKANA NA MALI IDHANIWAYO KUWA YA WIZI.TAREHE 17/07/2017 SAA 15.00  MJINI  KAHAMA  MKOA WA SHINYANGA ASKARI WA KIKOSI CHA UPELELEZI WALIMKAMATA OBADIA S/O MUNYA, MIAKA 32, MUHA, MKULIMA NA MKAZI WA MHONGOLO AKIWA ANAUZA PIKIPIKI YENYE USAJILI NAMBA T559 BEZ, ENGINE NAMBA SL157FMI * 16906998* NA CHASSIS NAMBA * LBRSPJB57G9004812* AINA YA SUNLG HUKU AKIWA NA KADI YA KUGHUSHI AKIUZIA PIKIPIKI HIYO. MTUHUMIWA ANAHOJIWA KWA KINA  NA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA. ZA  KUMFIKISHA  MAHAKAMANI HARAKA IWEZEKANAVYO ZINAFANYWA.

 (5)KUPATIKANA NA SILAHA AINA YA GOBORE (HOME MADE GUN)  TAREHE 17/7/2017  SAA 14:00  KIJIJI CHA SHISHINULU,KATA YA NSALALA,TARAFA YA ITWANGI,WILAYA/MKOA SHINYANGA  ASKARI POLISI WALIWAKAMATA WATU WAWILI (ME) WAKAZI WA KALIUA WAKIWA NA SILAHA/BUNDUKI TATU AINA YA GOBORE  ZINAZODAIWA KUTUMIKA KATIKA VITENDO VYA UHALIFU KWENYE MKOA WETU NA MIKOA JIRANI NA WALIKUWA WAKIZIPELEKA KWA MGANGA WA KIENYEJI ILI KUFANYIWA MATAMBIKO. UPELELEZI WA KINA UNAENDELEA NA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI. 

 IMETOLEWA NA MULIRO J MULIRO (ACP ) RPC-SHY

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post