IGP SIRRO AFANYA MABADILIKO MAKAMANDA WA POLISI,RPC MULIRO WA SHINYANGA AHAMISHIWA KINONDONI



Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Muliro Jumanne Muliro
****
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Saimon Sirro, amefanya mabadiliko ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni pamoja na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga.

Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Suzan Salome Kaganda amekuwa Mkuu wa kitengo cha Mafao na Fidia Makao Makuu ya Polisi, na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Murilo Jumanne Murilo ambaye alikuwa kamanda Polisi Mkoa wa Shinyanga.

Aidha, Nafasi ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga imechukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Simon Sylverius Haule, ambaye alikuwa Afisa Mnadhimu wa Polisi wa Mkoa wa Mara.

Uhamisho huo ni mabadiliko ya kawaida yanayotokea ndani ya Jeshi la Polisi katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.


Imetolewa na:

Barnabus D. Mwakalukwa - ACP

Msemaji wa Jeshi la Polisi.

Makao Makuu ya Polisi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post