Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI MWINGINE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 24 Mei, 2017 amemteua Bw. Tixon Tuliangine Nzunda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) - anayeshughulikia Elimu.


Kabla ya uteuzi huo Bw. Tixon Tuliangine Nzunda alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa.


Bw. Tixon Tuliangine Nzunda anachukuwa nafasi ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) - akishughulikia Elimu Bw. Bernard Makali ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa.


Uteuzi huu unaanza mara moja.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam


24 Mei, 2017

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com