Picha: BUKOBA YAKUMBWA NA MAFURIKO....MITUMBWI YATUMIKA KUOKOA WANANCHI

Faustine Ruta, Bukoba

ZAIDI ya watu 70 wameokolewa na Serikali baada ya kukumbwa na mafuriko yaliyotokana na mvua iliyoanza kunyesha kuanzia saa 9 usiku. 
Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo wakati alipo hojiwa na waandishi wa habari katika Kata ya Bakoba mtaa wa Nyakanyasi. 

Kinawilo alisema nyumba zote zilizoko kandokando ya mto Kanoni zote zimeathiriwa na maji kiasi kwamba wametumia mitumbwi ya uvuvi kuvusha watu. 


“Niseme tu mpaka sasa hakuna kifo chochote kile Zaidi ya vitu kuhalibika kwa kulowa maji”alisema kinawilo 
Aidha mkuu wawilaya alisema kuwa kuwa wananchi wachukue tahadhali pindi mvua zinapo nyesha tu watoke nje ya nyumba kwa usalama zaidi. 

Naye Josefati Bonge mkazi wa Omukigusha alisema kuwa katika nyumba yake hakuna kilichobakia kikiwa kizima.

“Kiukweli kuna kila sababu ya kuhama maeneo kama haya maana ni hatari kwa binadamu mfano’ waliokuwa wamelala fofo wana hali gani hivyo panatakiwa kuchukuliwa hatua mapema ili kuhamia sehemu stahiki”alisema Bonge .

Anitha Mziba mkazi wa Nyakanyasi alisema kuwa yeye katika familia yake hakuna alie umia Zaidi ya vitu vyote vyandani hakuna kilichotoka.

“Yani nimewabeba watoto wangu begani mmoja baada ya mwingine wakati huo mimi maji yakiwa yamenifikia kwenye shingo kwakweli ni hatari”alisema Mziba
Wakaazi wa hapa Tangu usiku saa 9 waliondoka!
Mkazi wa Omukigusha akisaidiwa kuvutwa juu baada ya kuanguka shimoni asubuhi leo kwenye mufda wa saa nne. Picha na habari na Faustine Ruta
Prince Motel


Crane Lodge and Tours
Hii ni nyumba ya Wageni...lakini inasemekana Usiku hawakupata usingizi kabisa!
Hivi ndivyo ilivyokuwa Asubuhi ya leo
Eneo la Ziwa Victoria...Ufukweni
Ufukweni Ziwa Victora
Patashika wakazi wakiokoa Nyasi kwa ajili ya Mifugo yao
Mkazi wa Nyakanyasi akivuka huku akiwa hana matumaini Aendako
Katikati ya Makazi ya watu Eneo la Nyakanyasi Mitumbwi imefanya kazi
Okoa okoa ikiendelea eneo la Nyakanyasi Mjini Bukoba leo hii

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post