Makubwa Haya! MWANAUME AATAMIA MAYAI YA KUKU ILI APATE VIFARANGA

Abraham Poincheval akiwa anatamia mayai katika makumbusho ya Paris

Msanii kutoka Ufaransa Abraham Poincheval anaendelea kuatamia mayai ya kuku akiwa na matumaini kwamba mwishowe yataangua vifaranga.

Msanii huyo anatumia joto kutoka kwa mwili wake kuatamia mayao hayo 10.

Poincheval ambaye hufanya uigizaji wa kuigiza mambo ya ucheshi lakini ya hatari tayari ameishi wiki mbili ndani ya dubu, miongoni mwa mambo mengine ya kushangaza.

Atakuwa katika chumba maalum ambacho anatamia mayai, ambapo watalii wanaweza kumtazama katka makumbusho ya Palais de Tokyo mjini Paris.

Anatarajia kutamia mayai hayo kwa siku 21 hadi 26.

"Kusema mweli, kimsingi, ni kama nimekuwa kuku," anasema.

Poincheval, 44, ameuita uigizaji huo wake - "Oeuf" (Yai kwa Kifaransa).

Badala ya kutamia mayai hayo kwa kuchutuma juu yake moja kwa moja, anatumia kiti maalum ambacho kina mfuko eneo lake la kukalia. Hapo ndipo mayai hayo yamewekwa.

Poincheval atakuwa amejifunga blanketi kuzuia joto kupotea.

Aidha, anapanga kula vyakula vinavyoongeza sana joto mwiliki, kama vile tangawizi.

Wakati wa haja, atatumia kijisanduku kidogo kilichomo mvunguni mwa kiti chake.

Ndipo mayai hayo yaangue vifaranga, hahitaji kuondoka zaidi ya dakika 30 kwa siku. Anapanga kutumia muda huo kula chakula.

Uigizaji wa sasa wa Poincheval anaufanya baada ya uigizaji wake aliouita "Pierre" (Jiwe kwa Kifaransa), ambapo aliishi ndani ya jiwe kubwa lililokuwa limechongwa sehemu ya kutoshea mwili wake ndani.Msanii huyo alikaa ndani ya jiwe kwa wiki mojaPoincheval pia alikaa wiki moja juu ya boriti ya urefu wa mita 20 nje ya kituo cha treni cha Gard du Nord mjini Parisalikaa pia siku 13 ndani ya dubualisafiri pia kwenye mto Rhone akitumia chpa kubwa ya plastiki iliyokuwa imefungwa kwa kifuniko. na aliishi ndani ya shimo wiki moja kwenye duka moja la vitabu Marseilles. Wakati mmoja, alitembea kutoka upande mmoja wa Ufaransa hadi mwingine bila kujipinda, akitumia dira kumuongoza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post