KUTANA NA ROBOTI YENYE UWEZO WA KUPAMBANA NA WAHALIFU KWENYE MADUKA MAKUBWA


Ubunifu ndio unaiendesha dunia lakini sio kila mtu amepewa uwezo wa kubuni bali wapo wachache kwenye kundi la wengi ambao wana uwezo wa kubuni mambo mbalimbali ndiyo maana nimekuletea stori hii ya ubunifu wa hali ya juu.

Kampuni ya Silicon Valley imebuni mbinu mpya ya kupambana na uhalifu katika maduka makubwa baada ya kutengeneza robot ambayo kazi yake ni kupambana na uhalifu katika maduka makubwa zikitengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu ambapo zitafanya kazi bila usimamizi wa binadam na kukodishwa kwa Dollar 7 (£5) ambazo ni sawa Tsh. 15,400 kwa saa.

Katika stori hii iliyochapishwa na mtandao wa Daily Mail April 27, 2017 ni kwamba robot inayoitwa Knightscope K5 ina urefu wa futi 5 ni maalum kufanya patrol katika maduka makubwa, viwanja vya michezo na kumbi za cinema kwa lengo la kuhakikisha usalama wa maeneo hayo.

Lengo kuu la kampuni hiyo ni kuzalisha maroboti wengi zaidi ambao watasambazwa duniani kote wakikusudia kupunguza uhalifu hadi 50% ambapo kwa mujibu wa ripoti ni kuwa wanakusudia siku moja zitumike na Polisi katika kusaidia kupambana na uhalifu.

Mmoja wa watengenezaji wa Knightscope Stacy Dean Stephens alisema: “Tunaanza na maeneo ya umma, hivyo tunaziruhusu kufanya patrol kwenye maeneo kama maduka makubwa, kampasi, viwanja vya michezo na nyumba za cinema.”

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527