Tanzia: Mpiga Picha wa Gazeti la Tanzania Daima Aliyepiga Picha za Mauaji ya Mwangosi Afariki Dunia

Mpiga picha wa gazeti la Tanzania Daima,aliyepiga picha za tukio la mauaji ya Daudi ya Mwangosi

Kuna taarifa kuwa mpiga picha wa gazeti la Tanzania Daima,aliyepiga picha za tukio la mauaji ya Daudi ya Mwangosi amefariki dunia.
 
Mwandishi Nguli nchini Tanzania Dotto Bulendu ameandika taarifa hii katika ukurasa wake wa Facebook:

"Simanzi,siku moja baada ya mahakama kuu kanda ya Iringa kumfunga miaka kumi na mitano askari ya aliyemuua Daudi Mwangosi,tasnia ya habari yapata pigo,mpiga picha wa gazeti la Tanzania Daima,aliyepiga picha za tukio la mauaji ya Daudi ya Mwangosi,SHUJAA JOSEPH SENGA,amefariki dunia usiku huu.

Senga amefia nchini India alikopelekwa kwa matibabu ya ugonjwa wa Moyo.

Bila Joseph Senga,shujaa aliyehatarisha maisha yake,akasimama bila woga,akapiga picha akiwa katikati ya msitu wa askari polisi wenye silaha,huku anga ikiwa imegubikwa na moshi wa mabomu ya machozi,milio ya risasi ikisikika,na kuzitunza,zikasaidia kufichua mauaji ya Mwangosi,leo hii asingekuwa Senga,nadhani kusingekuwa na kesi na mwisho hukumu dhidi ya aliyemuua Mwangosi.Nakulilia Senga..

Senga,Senga,Senga,Senga,umekwenda,Mungu aliamua akuweke hai mpaka hukumu itoke na mwisho amekuchukua,Senga umekwenda wadogo zako katika tasnia tukiwa na hamu ya kujifunza kutoka kwako.

Senga,Senga,kamsalimie Daudi Mwangosi,mwabie aliyemuua nae kahukumiwa jela miaka 15,kamwambie mazingira ya waandishi wa habari bado magumu.

Nenda Senga,picha zako zinabaki kuwa rejea ya mafunzo ya uandishi wa habari katika mazingira hatarishi"


Joseph Senga enzi za uhai wake..
Zifuatazo ni picha alizopiga wakati wa mauaji ya mwandishi wa habari wa Chanel Ten Daudi Mwangosi Septemba ,2012

Daudi Mwangosi akishambuliwa na askari polisi


Askari polisi wakiwa eneo la tukio


Masalia ya mwili wa Daudi Mwangosi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527