Simba Imempata Kocha wa Zamani wa Azam FC Joseph Omog


Klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba leo June 30 imetangaza rasmi kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii kuingia mkataba na kocha raia wa Cameroon Joseph Omog, Simba wametangaza kuingia mkataba na Omog bila kuweka wazi mambo kadhaa kwa kigezo kuwa taarifa rasmi itatoka kesho July 1.

Simba wameingia mkataba na Omog ambaye amewahi kuifundisha klabu ya Azam FC na kuipatia Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2013/2014 kwa mara ya kwanza, Omog kwa sasa ana umri wa miaka 44 na anatajwa kuwa kesho ndio atatambulishwa rasmi kujiunga na Simba.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527