Yanga Wamekubali Kipigo Hiki Dakika 90 za Mchezo Dhidi ya Al Ahly ya Misri



Siku moja baada ya kutolewa kwa klabu ya Azam FC katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika na klabu ya Esperance ya Tunisia, macho ya watanzania April 20 2016 yalielekezwa katika mchezo kati ya Yanga wawakilishi pekee katika michuano ya kimataifa dhidi ya Al Ahly ya Misri.


Yanga ambao mchezo wa awali uliochezwa Taifa Dar es Salaam walimaliza kwa sare ya goli 1-1, walienda Misri katika mji wa Alexandria kutafuta sare ya goli 2-2 ili waweze kufuzu au washinde mchezo huo kwa bahati mbaya Yanga wamekubali kipigo cha goli 2-1.

Klabu ya Al Ahly ya Misri ndiyo walianza kupata goli la uongozi kipindi cha pili, lakini Yanga walisawazisha dakika ya 57 kupitia kwa Donald Ngoma aliyetumia vyema krosi ya Juma Abdul, mambo yalizidi kubadilika zaidi kuanzia dakika ya 80 baada ya Al Ahly kuongeza nguvu ya kuishambulia kwa kasi na kufanikiwa kupata goli la ushindi dakika ya 95.

Kwa matokeo hayo Yanga wanakuwa wamerejea rekodi yao ya kufungwa na Al Ahly ya Misri, ambayo mwaka 2014 walifungwa tena katika hatua ya mikwaju ya penati 5-4 kwa nne. Yanga kwa sasa wanarudi kushiriki Kombe la shirikisho barani Afrika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post