Serikali Yawasilisha Bungeni Mpango Wa Maendeleo Ya Taifa kwa Mwaka Wa Fedha 2016/17 hadi 2020/21



Serikali imewasilisha bungeni mpango wa pili wa maendeleo ya taifa kwa mwaka fedha 2016/17 hadi 2020/21 ulioainisha vipaumbele vinne ikiwemo kujenga mazingira wezeshi ya uendelezaji biashara na uwekezaji pamoja na kukuza uchumi kwa kujenga msingi wa uchumi wa viwanda na kuwataka watanzania kufunga mkanda kuanzia mwaka ujao wa fedha. 
 
 
Kauli hiyo imetolewa na waziri wa fedha na mipango, Mhe Dkt Phillip Mpango baada ya kuwasilisha mpango huo bungeni ambapo amesema katika mwaka wa fedha ujao ili kufikia azma hiyo serikali imepanga kutumia asilimia 40 ya mapato yake katika miradi ya maendeleo ambapo amewataka watanzania kubadilika kujenga tabia ya kulipa kodi. 
 

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kuhusu mpango wa pili wa maendeleo ya taifa wabunge wamekuwa na mitazamo tofauti ambapo baadhi wameipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kuja na mpango wa unaoangalia maeneo muhimu katika ukuaji wa uchumi, huku wakionyesha kutoridhishwa na mpango huo. 
 

Aidha baadhi ya wabunge wamewataka wabunge kuanza kujadili vyanzo vya mapato vitakavyoweza utekelezaji wa mpango huo, huku wengine wakisisitiza kutokufanya hivyo kutarejesha yaliyofanyika katika mpango wa kwanza wa maendeleo ambapo mbaka sasa utekelezaji wake inaamika haujafikia zaisi ya asilimia 60.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post