Serikali Yakiri Upungufu Wa Sukari, Yaagiza Wafanyabiashara Walioficha Sukari Kushughulikiwa



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza maofisa biashara wa wilaya, mikoa na Taifa kukagua maghala yote ya wafanyabiashara walioficha sukari na kuwachukulia hatua.


Waziri Majaliwa alisema hayo leo asubuhi wakati akihitimisha mjadala wa hotuba ya mapato na matumizi ya ofisi yake na kuliomba Bunge likubali kupitisha.


Waziri Mkuu alisema ni kweli kwamba kuna upungufu wa sukari nchini, ingawa pia upo udanganyifu kwa baadhi ya wafanyabiashara.


Alisema takwimu kutoka kwa wataalamu zinaeleza kwamba mpaka sasa kuna tani 37,000 za sukari katika maghala nchini, lakini imekuwa haionekani kwa sababu wafanyabiashara wakubwa wameificha ili waiuze kwa bei kubwa.


“Ninawaagiza maafisa wa biashara kushughulikia suala hili, na kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika kuwa wamekwenda kinyume na taratibu tulizojiwekea,” alisema Majaliwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527