Kamishna Mkuu wa Zamani wa TRA na Wenzake Wawili Wanyimwa Dhamana


Baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kuondoa shitaka la utakatishaji fedha katika kesi inayowakabili Harry Kitillya, Shose Sinare na Sioi Solomoni, upande wa mashitaka umekata rufaa ya kupinga mwelekeo wa kuondolewa kwa shitaka hilo, anaandika Faki Sosi.


Kitillya, alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA); Sinare, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Uwezekezaji katika Benki ya Stanbic na Sioi Solomoni, Mwanasheria wa Benki ya Stanbic.


Amilis Mchaura, Hakimu Mkazi Kisutu amesema kuwa, shitaka la nane linalowakabili watuhumiwa hao lina upungufu kisheria hivyo mahakama italifuta shitaka hilo.

Jopo la mawakili wa upande wa utetezi linaongozwa na Dk. Lingo Tenga liliomba mahakama kuwapa wateja wao dhamana yenye masharti nafuu.


Baada ya Amilis Mchaura, Hakimu Mkazi kusimamisha kusikiliza kesi hiyo kwa dakika 30, aliporejea tu, Oswadi Tibabyekonya, Mwanasheria Mwandamizi wa Serikali alileta notisi ya rufaa kutoka Mahakama Kuu iliyokuwa ikipinga mwelekeo wa kufutwa kwa shitaka la utakatishaji fedha.


Hakimu Mchaura baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, alihailisha shauri hilo na kwamba, uamuzi atautoa tarehe 29 Aprili mwaka huu. Watuhumiwa wote wamekosa dhamana wamerudishwa rumande.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527