Picha 15!! MSANII RAY WA BONGO MOVIE AZUA GUMZO MTANDAONI,"KUNYWA MAJI MENGI UWE MWEUPE",TAZAMA PICHA HAPA UCHEKE SANA LEO

 
Msanii Baraka da Prince amejibu kauli ya Ray aliyoitoa hapo jana na kutoa siri ya yeye kubadilika rangi yake, na kusema kuwa anakunywa maji mengi na kufanya mazoezi sana.Akiongea na East Africa Television/ Radio, Baraka amesema kuwa kitu hicho ni mara ya kwanza kusikia maishani mwake, kwani hajawahi kusikia popote duniani.

Ameanza kwa kucheka....."hahahahahaaa, mi ndo mara yangu ya kwanza kusikia hiyo, sijawahi kusikia popote duniani, ila labda ni kweli (huu anacheka) ila mi sijui kama maji yanabadilisha rangi", alisema Baraka da Prince ambaye ni mweusi.

Baraka aliendelea kusema kwamba yeye haamini kabisa katika hilo na napenda rangi yake na hafikirii kubadilisha muonekano wake, kwani hivyo alivyo mashabiki wanampenda, licha ya Ray kusema pia anafanya hivyo ili awe na muonekano mzuri kwa jamii.

"Siamini hayo mambo, na napenda rangi yangu jinsi ilivyo, sasa kwa nini nibadlishe, siamini kama watu wanapenda rangi nyeupe, mi sina rangi lakini napendwa, naperform mpaka watu wanalia, mpaka napewa tuzo, kazi nzuri ndio inafanya mashabiki wapende kazi yako na wakukubali, mbona mi bonge la HB (akimaanisha handsome boy) na weusi wangu na watu weupe nawakalisha, mi handsome", alisema Baraka da Prince.

Akijibu post ya Godzila akimtaka Baraka da Prince akatumbukie baharini ili awe mweupe, amesema yeye na Godzila wanataniana, hivyo hana tatizo na hilo kwani pia anamchukulia kama kaka yake, hivyo haijamsumbua.

Angalia picha hapa ucheke sana leo
 
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post