BOMOA BOMOA YAANZA KWA KASI YA AJABU HUKO BARIADI SIMIYU



Zaidi ya nyumba 30 zimebomolewa mjini Bariadi chini ya usimamizi wa wakala wa barabara na jeshi la polisi, huku zoezi hilo likisimama kwa muda wa dakika 20 kufuatia mabishano makali na baadhi ya mmiliki wa nyumba akidai kutopewa notisi, mwingine kukataa kutoka ndani ya nyumba na kulazimika kutolewa kwa nguvu na askari polisi. 
 
 
Zoezi hilo ambalo limeanza majira ya saa kumi na mbili asubuhi huku likikumbana na vikwazo vya malumbano na baadhi ya wamiliki kugoma kubolewa nyumba zao kwa madai ya kutopewa notisi, huku nyumba hizo zikiwa na alama za X na baada ya dakika kadhaa zoezi hilo likaendelea. 
 

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Bariadi, Athuman Hamisi amekiri kuwa watu wote waliokuwa wanatakiwa kubomoa nyumba hizo walipokea barua za kubomoa ndani ya siku 30, huku baadhi ya umati uliofurika kushuhudia ukiunga mkono kufanyika zoezi hilo ambalo liko kisheria.
 

Akizungumzia zoezi hilo meneja wa Tanroad mkoa wa Simiyu Mhandisi Albert Kent amesema kuwa wametekeleza zoezi hilo kwa watu waliokaidi kubomoa ili kuweza kupisha shughuli za ukamilishaji wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Lamadi hadi mjini Bariadi unajengwa na kampuni ya kichina ya CCCC.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527