TAKUKURU YAMFIKISHA KIZIMBANI AFISA MTENDAJI WA MTAA KWA RUSHWA YA ELFU 30



Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoani Katavi imemfikisha Mahakamani Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Kawajense Manispaa ya Mpanda Catherine Kipeta kwa tuhuma za kumkamata za kushawishi na kuomba Rushwa ya Tsh 30,000.

Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi Christopher Nakua aliwaambia waandishi wa Habari jana kuwa Afisa Mtendaji huyo alikamatwa January 18 mwaka huu katika eneo la Mtaa wa Kawajense mjini Mpanda.

Alisema mtuhumiwa alikamatwa kufuatia Ofisi ya Takukuru kupokea taarifa kutoka kwa msiri wao aliyemtuhumu Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Kawanjense Catherine Kipeta kuwa amemwomba na kumshawishi ampe Rushwa ya kiasi cha Tsh 30,000 ili asiweze kumpeleka kwenye Baraza la Kata kwa kosa la kufungua sehemu yake ya biashara katika muda wa kufanya usafi .

Baada ya kupokea taarifa hizo ofisi ya Takukuru ilifanya uchunguzi na baada ya kuthibitika kuwepo kwa tuhuma hizo ndipo mtego wa Rushwa ulipoandaliwa na walipoweza kumkamata Catherine Kipeta ambaye ni Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Kawajense baada ya kuwa amepokea Rushwa aliyokuwa ameiomba kutoka kwa msiri huyo.

Nakua aliwaeleza waandishi wa Habari kuwa mshitakiwa alifikishwa juzi katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda na kufunguliwa kesi No.CC 12- 2016.

Na mtuhumiwa alisomewa mashitaka ambayo ni kuomba Rushwa ya fedha tasilimu Tsh 30,000 shitaka la pili alilosomewa ni kupokea Rushwa ya shilingi elfu thelasini kinyume na matakwa ya mwajiri wake kifungu cha 15 (1) (a) cha sheria ya kuzuia na kupambana na RushwaNa 11 ya mwaka 2007.

Takukuru Mkoa wa Katavi wametowa wito kwa wananchi wote wajiepushe na vitendo vya Rushwa ambavyo hupelekea kutopatikana kwa haki , kutowajibika kwa watumishi wa umma na kwenda kinyume na maadili ya kanuni na viapo vya utumishi.
Na Walter Mguluchuma-Malunde1 blog Katavi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527