Picha 21!! WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA WAIBUKIA KWENYE KIWANDA CHA MAFUTA CHA WACHINA,JIELONG HOLDINGS (T) LTD

Waandishi wa habari wakielekea katika
Kiwanda cha Mafuta ya kula ya Alizeti na Pamba cha Jielong Holdings(T) LTD kilichopo katika eneo la Nhelegani manispaa ya  Shinyanga katika ziara yao kujionea jinsi kinavyofanya shughuli zake na kusikiliza malalamiko mbalimbali kutoka kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho.

Nje ya kiwanda cha Jielong Holdings(T) LTD



Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga wakiwa ndani ya kiwanda cha Jielong Holdings(T) LTD,wa pili kutoka kushoto ni afisa utawala wa kiwanda hicho Joseph Francis Warioba akiwaongoza waandishi hao wa habari
Afisa utawala wa kiwanda chaJielong Holdings(T) LTD Joseph Francis Warioba akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari



Mwandishi wa habari wa Channel Ten John Mponeja akiuliza swali kwa mkurugenzi wa kiwanda cha Jielong Holdings(T) LTD bwana Jerry Qi



Afisa utawala wa kiwanda cha Jielong Holdings(T) LTD Joseph Warioba akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu namna wanavyopakia mafuta baada ya uzalishaji huku akiongeza kuwa hivi sasa wamesimamisha uzalishaji wa mafuta ya pamba na alizeti kutokana na kukosa malighafi



Mafuta ya kupikia yakiwa tayari kupelekwa kwa walaji



Afisa utawala wa kiwanda cha Jielong Holdings(T) LTD Joseph Warioba akionesha sabuni inayotengezwa katika kiwanda,hicho kwani mbali na kuzalisha mafuta ya kula,mabaki ya malighafi huyatumia kutengeneza sabuni maarufu kwa jina la Gwanji



Afisa utawala wa kiwanda cha Jielong Holdings(T) LTD Joseph Warioba akionesha gwanji



Shughuli ya kutengeneza ndoo inaendelea kiwandani hapo



Wanatengeneza ndoo.....



Tunatengeneza ndoo na kuweka lebo kwenye ndoo.....



Viongozi wa kiwanda cha  Jielong Holdings(T) LTD Joseph Warioba wakionesha mafuta ya kupikia kwa waandishi wa habari



Mkurugenzi wa kiwanda cha Jielong Holdings(T) LTD Joseph Warioba akiwaeleza jambo waandishi wa habari,Marco Maduhu na Kadama Malunde(kulia)



Waandishi wa habari wakiwa ndani ya  kiwanda cha Jielong Holdings(T) LTD wakiwa na viongozi wa kiwanda hicho


Afisa utawala wa kiwanda cha Jielong Holdings(T) LTD Joseph Warioba akizungumza na waandishi wa habari



Mkurugenzi wa kiwanda cha Jielong Holdings (T) LTD Jerry Qi akizungumza na waandishi wa habari


Waandishi wa habari wakizungumza na viongozi wa kiwanda cha  Jielong Holdings(T) LTD Joseph Warioba



Kulia ni afisa mahusiano wa kiwanda cha Jielong Holdings(T) LTD Lilian Sisawa,kushoto ni mwandishi wa habari Chibura Makorongo



Waandishi wa habari wakizungumza na viongozi wa wa kiwanda hicho

Jengo la utawala la kiwanda cha Jielong Holdings(T) LTD

Kiwanda cha Mafuta ya kula ya Alizeti na Pamba cha Jielong Holdings(T) LTD kilichopo katika manispaa ya Shinyanga kinakabiliwa na ukosefu malighafi hali inayosababisha kisifanye uzalishaji na kuleta changamoto ya ajira kwa wakazi wa Shinyanga.


Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya waandishi wa habari kufanya ziara katika kiwanda hicho mkurugenzi wa kiwanda hicho Jerry Qi alisema kutokana na uhaba wa malighafi za kuzalishia mafuta hayo wanalazimika kuzima mitambo yao.


Qi alisema hivi sasa zoezi la kutengeneza mafuta linasuasua kutokana na kukosa malighafi hizo huku akitoa wito kwa wakulima nchini kupeleka alizeti na pamba yao katika kiwanda hicho.


Katika hatua nyingine Qi alitaja changamoto nyingine wanayokabiliana nayo kuwa ni pamoja na mtazamo hasi kwa wananchi juu ya kiwanda hicho kwani kuna uzushi unaoenezwa kuwa hawatoi mikataba kwa wafanya kazi wao.


Kwa upande wake afisa Utawala wa Kiwanda hicho Joseph Warioba alikanusha madai ya baadhi ya wafanya kazi wa kiwanda hicho wakiwemo madereva kuwa wamekuwa wakinyanyaswa na viongozi wa kiwanda hicho ikiwemo kufanyishwa kazi zaidi ya wa muda wa kazi na mikataba yao.


Warioba alisema kiwanda hicho kimekuwa kikitoa mikataba kwa kuzingatia sheria za nchi na kwa upande wa madereva wa magari wamekuwa wakiwakata mishahara yao hasa pale wanapokiuka sheria za barabarani na kutozwa faini mfano wanapoendesha magari kwa mwendo kasi.


“Kinachotusumbua hapa ni wafanya kazi kutokuwa na elimu ya kutosha,mambo mengi hawaelewi,kuna wengine ukiwakata pesa za mifuko ya kijamii mfano NSSF,wanagoma kufanya kazi wakati kiutaratibu wanapaswa kujiunga na mifuko hiyo,wengine hawafiki kabisa kazini tena bila taarifa lakini anataka alipwe”,alieleza Warioba.


Hata hivyo wafanya kazi wa kiwanda hicho waliozungumza na gazeti hili waliogoma kutaja majina yao wakiogopa kuhatarisha ajira zao walisema wamekuwa wakinyanyaswa ikiwemo kupigwa,kukatwa mishahara yao bila sababu zinazoeleweka,ikiwemo kuchelewa kazini ingawa kiwanda hakina magari kwa ajili ya kuwasafirisha na huwa wanatumia gharama zao kusafiri.


Walisema madai mengine ni kutolipwa pesa za likizo,kutotibiwa wanapougua,kutopewa ruhusa hata kama umefiwa,madereva kukatwa sehemu ya mishahara yao hasa pale gari linapoharibika ikiwemo matairi kuisha,pesa kidogo wakati wa safari ndefu,mishahara midogo wanayolazimika kugawana na makondakta wao.

Na Kadama Malunde-Malunde1 blog Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527