ANGALIA PICHA- RAIS MAGUFULI AMTEMBELEA MAMA MARIA NYERERE KUMFARIJI KUHUSU KIFO CHA LETICIA NYERERE


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 11 Januari, 2016 amemtembelea na kumpa pole mke wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere kufuatia kifo cha Mkwewe Leticia Nyerere kilichotokea jana huko Maryland Marekani alikopelekwa kwa ajili ya kupata matibabu mapema mwezi huu.


Pamoja na kutoa mkono wa pole kwa Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Msasani Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli pia amewapa pole wanafamilia wote na amewaomba kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na ndugu yao.

Msemaji wa familia ya Mwalimu Nyerere Bwana Joseph Butiku amemueleza Rais Magufuli kuwa familia inaendelea na taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka nchini Marekani na itatoa taarifa baadaye.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Mama Maria Nyerere kufatia kufiwa na Mkwe wake Bi Leticia Nyerere aliyefariki huko nchini Marekani. Rais alikwenda nyumbani kwa Baba wa Taifa Msasani Dar es salaam kumpa pole Mama nyerere Januari 11,2016


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapa pole wanafamilia alipofika nyumbani kwa Baba wa Taifa Msasani Dar es salaam kumpa pole Mama nyerere Januari 11,2016



Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipata maelezo juu ya uataratibu wa msiba kutoka kwa mwanafamilia Joseph Butiku

Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na wanafamilia

Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana na Mama Maria Nyerere, Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na wanafamilia alipokwenda nyumbani kwake Msasani kumfariji kufuatia kifo cha Mkwe wake Marehemu Leticia Nyerere huko Maryland, Marekani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527