ANGALIA PICHA_HIVI NDIVYO MAGUFULI ALIVYOITIKISA RUVUMA,MAELFU YA WATU WAJITOKEZA KUMSIKILIZA
Tuesday, September 01, 2015
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Songea waliokuwa wamefurika kwenye uwanja wa Maji Maji mjini humo mkoani Ruvuma,Mgombea huyo ambaye anawaomba Watanzania ridhaa ya kuwaongoza katika awamu ya tano. Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wakazi wa mji wa Songea, ambapo alisema katika serikali yake wakulima hawatokopwa mazao yao, mbolea zitapatikana kwa wakati, barabara zitaboreshwa ,elimu bure mpaka kidato cha nne, kuongeza maslahi ya walimu pamoja na kuboresha huduma za afya.
Mgombea Ubunge Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama akipokea Ilani ya Uchaguzi ya CCM kutoka kwa Mgombea Urais kupitia chama hicho, Dk Magufuli wakati wa mkutano huo wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Tamasha mkoani Ruvuma. Dk Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Nyasa, Stelah Manyanya katika mkutano wa kampeni katika Mji wa Lituhi,ambapo pia alimkabidhi Ilani ya chama hicho.
Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi mgombea ubunge wa Jimbo la Mbinga Ndugu Sixtus Mapunda kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mbinga mjini. Dk Magufuli akishuka kwenye Kivuko cha Mto Ruhuhu akitokea Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe kwenda Mbinga mkoani Ruvuma kuendelea na kampeni za urais ubunge na udiwani. Dk Magufuli ameahidi kujenga daraja la mto huo.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mkazi wa mji wa Peramiho ambaye ni mlemavu wa ngozi,jioni ya leo mara baada ya kumaliza kuwahutubia wananchi wa mji huo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni. Dk Magufuli akimsalimia mmoja wa walemavu waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni mjini Mbinga.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCm Dk. Emmanuel Nchimbi akihutubia wakazi wa Songea mjini ambapo aliwataka wananchi hao kumpa kura nyingi Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli kwenye uchaguzi utakaofanyika Oktoba 25,kwa sababu ni Muaminifu,muadilifu na ni mchapa kazi. Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Ndugu William Lukuvi akihutubia wakazi wa Songea mjini kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Maji Maji jana jioni. Maelfu ya Wananchi wakiwa wamefurika ndani ya uwanja wa maji maji mjini Songea jana jioni kwenye mkutano wa kampeni wa CCM,mkoani Ruvuma jioni ya leo,ambapo Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe aliwahutubia wananchi hao. Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Mbinga. Waanchi wakifuatilia hotuba ya Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Tamasha-Peramiho mkoani Ruvuma jana jioni. Wananchi wakishangilia Umati wa wakazi wa Peramiho wakisikiliza hotuba ya Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni katika uwanja wa Tamasha ndani ya jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma. Baadhi ya Wananchi wa Peramiho wakifurahia jamo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni. Mgombea urais wa Tanzania kupitiaa CCM,, dK John Magufuli akiwa na watoto aliowapatia zawadi alipokuwa akiondoka baada ya kujinadi katika Jimbo la Peramiho, mkoani Ruvuma Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wakazi wa Mbinga. Wananchi wakishangilia jambo kwenye mkutano wa kampeni za ccm jana jioni ndani ya uwanja wa Maji Maji mjini Songea.
Wananchi wa Songea mjini wakishangilia jambo wakati mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa Maji maji mjini humo.
********************* Mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dr John Pombe Magufuli amepata mapokezi makubwa katika mkoa wa Ruvuma na kuahidi kuwa katika kipindi chake cha uongozi Tanzania itakuwa nchi inayotegemea uchumi wa viwanda na maliasili pamoja na kutoa fursa za uwekezaji wenye tija kwa taifa kwa wawekezaji wazalendo na wa kigeni.
Dr Magufuli ametoa ahadi hiyo na kuwataka watanzania kumuamini kwa kuwa anamaanisha kile anachokiahidi kwa kuwa anamuogopa mungu na kuongeza kuwa anatamani kuiona tanzania inayotegemea uchumi wa viwanda na maliasili badala ya kuwa na lundo la kodi kero kwa wananchi na kwamba atatoa fursa na upendeleo maalum kwa wawekzaji wazawa lakini pia wageni ili kuwa na uwekezaji wenye tija kwa taifa.
Akizungumza na umati wa wananchi waliojitokeza katika uwanja wa majimaji kusikiliza sera za Dr Magufuli aliyekuwa mbunge wa Songea mjini Dr Emmanuel Nchimbi amewataka watanzania kumchagua Dr Magufuli kwa kuwa ndie kiongozi pekee anayeahidi na kutekeleza.
Akitokea mkoani Njombe kuingia mkoani Ruvuma ambapo ametumia kivuko kuvuka mto ruhuhu ambapo wananchi wamelalamika kupoteza maisha kwa kuliwa na mamba wakati wa kuvuka mto huo lakini pia wananchi wa mbinga wakimtaka kutafuta masoko yenye uhakika kwa ajili ya mazao yao.
Akijibu kero hizo Dr Magufuli amesema endapo atachaguliwa kuwa rais wa awamu ya tano itakuwa ni marufuku kwa serikali yake kukopa mazao kwa wakulima na kwamb watalipwa papo kwa hapo lakini pia akaahidi kujenga daraja katika mto ruhuhu.
Jumanne ya Septemba mosi Dr Magufuli anatarajiwa kuendelea na ziara yake ya kujinadi kwa watanzania kupata fursa ya kuliongoza taifa la tanzaia mkoani mtwara.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin