Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MHESHIMIWA LOWASSA AFANYA KWELI HUKO NJOMBE..


Mgombea urais wa vyama vinavyounda UKAWA Mh Edward Lowassa ameendelea kunadi sera zilizoko kwenye ilani ya umoja wa vyama vyao katika wilaya za mkoa wa Njombe huku wananchi, viongozi, na wagombea wa UKAWA wakiwataka watanzania kutambua kuwa hatua ya wagombea wa CCM ya kuendelea kulalamika na kutoa ahadi ni kielelezo cha kutosha kuonyesha kuwa hawana jipya na wamepoteza sifa za kuongoza.



Wakizungumza katika mji wa Makambako mgombea ubunge wa jimbo la Lupembe Bw Edwin Swai amesema kuendelea kuwasikiliza viongozi wagombea wa CCM wakitoa ahadi hewa na kulalamika bila kuchukua hatua ni kuwaona watanzania kuwa dhihirishia watanzania kuwa hawajui wanachokifanya.

Waliowahi kuwa mawaziri mkuu wa serikali ya CCM Mh Fredrick Sumaye na waziri wa mambo ya ndani Laurence Masha ambao wamehamia UKAWA wakaendelea kuweka wazi umuhimu wa watanzania kupokea mabadiliko.

Ukafika wakati wa Mh.Lowassa kueleza sera zilizoko kwenye ilani ya UKAWA na namna alivyojipanga kuwatumikia watanzania kama wakimchagua kuwa rais likiwemo la kuondoa tabaka la maskini na tajiri Mh Lowassa pia awahakikishia watanzania suala la amani.

Baadhi ya wananchi wamesema baada ya kusikia sera za UKAWA wana matumaini makubwa ya kuondokana na matatizo waliyonayo chini ya Mh Edward Lowassa ambaye wanajua utendaji wake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com