ZAIDI YA WAFUGAJI 300 WA CCM, WAZICHOMA KADI ZAO NA KUHAMIA CHADEMAZaidi ya wanachama mia 300 waliokuwa chama cha CCM kutoka jamii ya kifugaji katika kata ya Engaruka wilaya ya Monduli wamezichoma kadi zao za CCM na kujiunga na CHADEMA huku wakidai maamuzi yao yametokana na utashi wao binafsi kwa kuzingatia hali halisi ya kisiasa ilivyo hivi sasa

Mamia ya wanachama walikusanyika katika mkutano wa hadhara kukusanya kadi za CCM kuzichoma moto na kuchukua kadi za CHADEMA.


Akizungumza baada ya kuwapokea wanachama hao akiwemo mwenyekiti wa kijiji cha Engaruka Lewanga Kivuyo mwenyekiti wa Bavicha wilaya ya Monduli Yasini Shabani amesema Chadema ni chama kinacho zingatia haki ya kila binadamu na kila mwanachama.

Kada maarufu wa Chadema Julias Karanga amewataka wananchi kuwa wavumilivu kwa kuwa mabadiliko yana changamoto nyingi za kukatisha tamaa kutoka kwa mahasimu lakini kwa nguvu ya mungu watayashinda.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post