ANGALIA VIDEO WANAWAKE WAKIENDESHA BAISKELI WAKIWA NA NDOO ZA MAJI KICHWANI SHEREHE ZA NANE NANE SHINYANGA




Washirikiwa mbio za baiskeli kundi la akina mama wanaoendesha baiskeli wakiwa wamebeba ndoo kichwani wakijiandaa kuanza shindano hilo katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga leo wakati wa sherehe za wakulima maarufu Sherehe za Nane Nane zilizohusisha mashindano ya mbio za baiskeli washiriki kutoka kanda ya ziwa yaliyodhaminiwa na kampuni ya bia Tanzania (TBL)kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager.Akina mama hao zaidi ya 10 waliendesha walizunguka uwanja wa Kambarage mara 10(Km 4) bila kuanguka wala kuangusha ndoo za maji-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog




Mashindano yakiendelea,ndoo kichwani,speed ya ajabu...



Mshindi wa kwanza Stella Nganga akimaliza mbio hizo .....



Washindi wa kwanza hadi wa tatu mbio za baiskeli za akina mama wakiwa wamebeba ndoo za maji kichwani wakiwa katika picha ya pamoja,kushoto ni mshindi wa kwanza ni Stella Nganga kutoka Maganzo,Shinyanga,katikati ni Christina Richard kutoka Masekelo Shinyanga na Elizabeth Shuli kutoka Lubaga Shinyanga.

ANGALIA HAPA CHINI.VIDEO WANAWAKE WAKIENDESHA BAISKELI WAKIWA NA NDOO ZA MAJI KICHWANI

 Video ya Kwanza wanawake wakijiandaa na baiskeli zao



Video ya pili wanawake wakiendesha baiskeli na ndoo za maji kichwani

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post