Maajabu Haya!! NG'OMBE WAANDAMANA HADI KWENYE MADUKA MJINI KISA MAZIWA!!




Ushawahi kukutana na ngo'mbe katika maduka ya jumla?

Na ushawahi kusikia maandamano yanayojumuisha ng'ombe ?

Amini usiamini wanunuzi katika maduka ya kifahari katika mji ya Asda Queensway, Stafford Uingereza walipigwa na butwaa ng'ombe walipoingia dukani humo !

Yamkini mifugo hao waliletwa humo na wakulima waliokuwa wakiandamana kupinga bei duni ya maziwa wanayolipwa na uongozi wa maduka hayo ya jumla.



Wakulima 70 wakiandamana na ng'ombe wawili walishiriki katika maandamano hayo ya kipekee.

Mnunuzi mmoja Adam Williams aliiambia BBC kuwa hata wahudumu wa duka hilo hawakuficha mshangao uliowakumba.

Walipigwa na butwaa wote ng'ombe walipoingia dukani!''

Walisababisha hali ya mshikemshike kwani walifululiza hadi upande wa ndani kabisa ya duka hilo!''

Wakulima hao wanataka maduka hayo ya jumla yawaongezee bei ya maziwa ili na wao waweze kujikimu kimaisha.

Hata hivyo wasimamizi wa maduka hayo ya jumla wanasema kuwa hilo halitafanyika.

Wanadai kuwa hakuna uhusiano wowote wa bei ya juu ya maziwa katika maduka yao na bei duni wanayolipwa wakulima shambani.

Mkulima mmoja kutoka Stafford Matthew Weaver, amenukuliwa akisema

"Tulijua kuwa iwapo tunataka kupata ufanisi katika maandamano yetu ilikuwa lazima tufanye kitu cha kipekee ambacho pia kitawavutia watu na kuwapa sababu ya kuwachekesha.''

Weaver alisema wafugaji hao walitokea Derbyshire, Shropshire na Warwickshire .

Alisema kuwa bado wanapanga maandamano mengine katika maduka zaidi.

Kampuni ya maziwa ya Muller ilitangaza kuwa itapunguza bei ya maziwa kwa sababu soko lake limeporomoka

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post