Mambo ya Ajabu!! SHINDANO LA KUNG'ATWA MBU,MSHINDI ANAPATA MSICHANA MREMBO ZAIDI
Mbu wanajulikana kwa kuwa adui namba moja wa binadamu kutokana na kusababisha malaria… pengine hili lililotokea Russia linaweza kukushangaza na kukushtua kidogo.

Katika mji wa Perm wameamua kila mwaka kusherehekea tamasha la kipekee la mashindano ya kuchagua msichana mrembo zaidi ambapo watashindanishwa kwa kuvaa nguo fupi na atakayekuwa na alama nyingi za kuumwa na mbu baada ya kusimama kwa dakika zipatazo 20 katika eneo lenye mbu wengi ataibuka mshindi.


Mmoja wa washiriki akiwa na muonekano wa mbu

Shindano limeandaliwa na Natalya Paramonova litasimamiwa na majaji wakiwemo madaktari ambao watakagua miili yao na msichana atakayekuwa na alama nyingi za kuumwa na mbu ndiye atakuwa mshindi.

Shindano hilo pia liliwahi kufanyika mwaka 2013 huku mshindi akiwa na alama za kuumwa na mbu mara 100.

Mbali na shindano hilo pia lipo la kushika mbu akiwa hai.

Icheki video ya hii stori hapa, lugha inayoongelewa ni ya Russia kwa hiyo unaweza tu kucheki kinachoendelea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post