MREMBO HUYU AJITOSA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA KISHAPU,ANGALIA PICHA AKICHUKUA FOMU OFISI ZA CCM MKOA WA SHINYANGA

Hapa ni ndani ya ofisi ya Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga ambako leo Bi Radhia Kalombola(pichani) ambaye ni mjumbe wa Baraza la Vijana wilaya ya Kishapu amechukua fomu ya kuwania ubunge wa Viti Maalum kundi la Vijana kupitia CCM katika jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga.

Mtia nia huyo ya Ubunge mwenye shahada ya Sayansi na Siasa,ambaye ni kada mkubwa wa CCM alifika katika ofisi za CCM na kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo kwa katibu wa UVCCM Teddy Athumani huku mtia nia huyo akisindikizwa na wapambe wake.

Radhia Kalombola baada ya kuchukua fomu ya kuwania ubunge wa viti maalum Julai 16,2015 asubuhi ,alirudisha fomu hiyo Julai 16,2015 mchana baada ya kukamilisha taratibu zote zinazotakiwa.

Akizungumza na Malunde1 blog Kalombola alitoa wito kwa vijana katika jamii kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu kwani ni muda mzuri kwa vijana kushika uongozi kwa ajili ya kuendeleza chama na mafanikio ya vijana katika jamii.

Katika hatua nyingine aliwaasa vijana kujitafakari na kujipima kwa kina kabla ya kutaka kugombea nafasi za uongozi kwa kuangalia matendo yao ya siku za nyuma kwani kiongozi ni kioo cha jamii.

Kalombola alisema vijana wengi wamekuwa wajiingiza katika mambo ya siasa bila kufikiria vitendo vyao vya nyuma vitendo ambavyo vinaharibu sifa ya chama.

“Naomba vijana wenzangu waangalie vitendo vyao vya siku za nyuma kabla ya kutaka uongozi,kwani kiongozi kama ana tabia mbaya anaharibu sifa ya chama”,aliongeza Kalombola.

“Kiongozi anatakiwa awe na sifa na vigezo,angalau awe na upeo na sifa nzuri,kama unaingia halafu una sifa mbaya sidhani kama italeta maana kwa watu ambao wanakutazama kwani kiongozi anatakiwa kuwa mfano wa kuigwa katika jamii”,alieleza Kalombola.

Malunde1 blog ilikuwepo eneo la tukio,mwandishi wetu Kadama Malunde ametuletea picha 19,Angalia hapa chini.Ni SAA NNE ASUBUHI JULAI 16,2015-Kushoto ni Radhia Kalombola akiwa na baadhi ya wapambe wake wakiwasili katika ofisi ya katibu wa UVCCM mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuchukua fomu ya kuwania ubunge wa viti maalum kundi la Vijana jimbo la Kishapu mkoa wa Shinyanga


Kushoto ni Radhia Kalombola akiwa na baadhi ya wapambe wake wakitafakari jambo kabla ya kuingia kwenye ofisi ya UVCCM mkoa wa Shinyanga

Kulia ni Kijana Radhia Kalombola ambaye ni mjumbe wa Baraza la Vijana CCM wilaya ya Kishapu akipata maelekezo kutoka kwa Katibu wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Teddy Athumani (katikati) na katibu muhtasi ofisi ya katibu wa UVCCM bi Regina Shija kabla ya kuchukua fomu ya kuwania ubunge wa Viti Maalum kundi la Vijana katika jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga.

Baadhi ya wapambe wa Radhia Kalombola wakiwa katika ofisi ya katibu wa UVCCM mkoa wa Shinyanga

Kushoto ni Katibu wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Teddy Athumani akitoa maelekezo kwa Radhia Kalombola kuhusu fomu za ubunge wa viti maalum kundi la vijana

Radhia Kalombola(wa pili kulia) akiwa ndani ya ofisi ya UVCCM mkoa wa ShinyangaKatibu Muhtasi akiandaa fomu kwa ajili ya kumkabidhi Kijana Radhia Kalombola.Pichani ni Katibu wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Teddy Athumani (katikati) na katibu muhtasi ofisi ya katibu wa UVCCM mkoa bi Regina Shija


Radhia Kalombola akikabidhiwa fomu ya kuwania ubunge wa viti maalum kundi la vijana jimbo la Kishapu mkoani ShinyangaRadhia Kalombola akionesha fomu ya kuwania ubunge viti Maalum kundi la vijana jimbo la KishapuKijana Radhia Kalombola akijiandaa kupokea fomu ya kuwania ubunge wa Viti Maalum kundi la vijana jimbo la Kishapu


Radhia Kalombola akipongezwa baada ya kuchukua fomu kuwania ubunge wa viti maalumu kundi la vijana jimbo la Kishapu mkoani ShinyangaRadhia Kalombola akipongezwa baada ya kuchukua fomu kuwania ubunge wa viti maalumu kundi la vijana jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga


Ni Saa Nane Mchana,Julai 16,2015-Radhia Kalombola anarudisha fomu ya kuwania ubunge wa viti maalum kundi la Vijana jimbo la KishapuRadhia Kalombola anarudisha fomu ya kuwania ubunge wa viti maalum kundi la Vijana jimbo la KishapuRadhia Kalombola anarudisha fomu ya kuwania ubunge wa viti maalum kundi la Vijana jimbo la Kishapu kwa katibu muhtasi ofisi ya Katibu wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Regina ShijaRadhia Kalombola na wenzake wakiondoka kwenye ofisi za UVCCM mkoa wa Shinyanga katika jengo la NSSF mjini Shinyanga baada ya kukamilisha zoezi la kuchukua fomu na kurudisha fomu ya kuwania ubunge wa viti maalum kundi la vijana jimbo la KishapuMwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga Mjini Shella Mshandete akimpa mkono wa hongera kijana Radhia KalombolaNje ya jengo la CCM mkoa wa Shinyanga baada ya kumaliza zoezi la kuchukua na kurudisha fomuBwana Nicholaus akimpa mkono Radhia Kalombola


Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog- Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post