MWANDISHI ANUSURIKA KUDONDOKA UKUMBINI KWA KIHORO CHA UCHAGUZI GEITA


Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Geita(Geita Press Club-GPC)imepata uongozi mpya baada ya uchaguzi kufanyika kwa mjibu wa katiba ya klabu hiyo,huku mgombea nafasi ya uenyekiti akinusurika kuanguka ukumbini wakati wa kuhesabu kura na kuomba awashiwe kiyoyozi ili kumnusuru.

Uchaguzi huo uliosimamiwa na Victor Maleko kwa niaba ya umoja wa vyama vya waandishi wa habari Tanzania(UTPC),ulishuhudia David Azaria akiibuka mshindi kwa nafasi ya uenyekiti,aliyepata kura 13 dhidi ya Peter Makunga aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo aliyepata kura 7 ambaye alimanusra aanguke ukumbini kwa kihoro wakati kura zikihesabiwa na kuomba awashiwe kiyoyozi kumnusuru.

Wanachama wa 20 wa GPC walimchagua pia Victor Bariety,kuwa makamu Mwenyekiti kwa kura  10 kati ya kura 20 zilizopigwa akimshinda mpinzani wake  Ester Sumira aliyepata kura 9 huku moja ikiharibika.

Katika uchaguzi huo,Salum Maige aliyekuwa mgombea pekee,alichaguliwa kwa kura 15 kati ya kura 20 zilizopigwa 3 za hapana na 2 ziliharibika kuwa katibu mkuu huku nafasi ya katibu msaidizi ikichukuliwa na Marco Kanani aliyepata kura 11 dhidi ya mpinzani wake Jackline Masinde aliyepata kura 8 na 1 kuharibika.

Wanachama hao walimchagua Anna Ruasha aliyekuwa mgombea pekee kuwa mweka hazina kwa kura  14,kati ya kura 20 zilizopigwa huku kura 2 zikiharibika.

Kwa mjibu wa katiba ya klabu hiyo,wajumbe watatu wa kamati tendaji walichaguliwa ambao ni Yohana Bukombe,Alex Sayi na Ernest Magashi.
Viongozi hao kwa nyakati tofauti waliomba ushirikiano wa wanachama kwa ajili ya kuboresha utendaji wa shughuli za uandishi wa habari na maisha ya wanatasnia hiyo wa mkoani Geita.

Awali kabla ya matokeo hayo kutangazwa wakati kura zikihesabiwa Makunga ambaye alikuwa akiomba nafasi ya uenyekiti aliwavunja mbavu wajumbe wa mkutano huo pale alipoomba awashiwe kiyoyozi muda mfupi baada ya kura kuanza kuhesabiwa akidai hajisikii vizuri na alipowaszhiwa kiyoyozi alidai amerejea kwenye hali yake ya kawaida jambo ambalo liliibua vicheko kwa baadhi ya wajumbe.

Na Victor Bariety- Malunde1 blog Geita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post