JAMAA ALIKIMBIA BEGI LAKE LA BANGI NDANI YA BASI WAKATI WA KUCHIMBA DAWA
Mara nyingi tunasikia stori kuhusu watu kukamatwa na dawa za kulevya kwenye viwanja vya ndege, wapo wanaotoka TZ kwenda nje na wapo wanaokamatwa wanaziingiza pia kutoka nje ya nchi.. nina hii stori kutoka ITV kuhusu mtu kukutwa na bangi ndani ya basi.
Basi la Maning’i nice lilitoka Mtwara kwenda Dar, njiani kulikuwa na Checkpoint ya Polisi ambapo jamaa aliyebeba bangi kwenye begi aliomba akajisaidie, Polisi walipoingia kwenye gari kukagua wakakutana na begi hilo lililojaa bangi na jamaa mwenye nalo alikuwa ameshakimbia tayari.
“Kuna mtu mmoja aliteremka akasema ana mkojo.. Askari akauliza nani mwenye hili begi yule jamaa akaanza kukimbia vichakani. Askari wakakimbizana nae maporini, akatokomea“– amesimulia dereva wa basi hilo, Hashim Mohamed.


Bangi iliyokutwa kwenye begi hilo ina uzito wa kama kilo 25 hivi… 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post