Mh Hii Kali!! MWANAMKE AJIFUNGUA BILA KUJUA BARABARANI,MTOTO AOKOTWA

born

Kesi za wanawake kushindwa kutambua muda wao wa kujifungua unapofika zimekuwa zikitokea mara kwa mara na hata wengine kushindwa kujitambua kama ni wajawazito hadi pale unapokaribia wakati wa kujifungua.

Kuna hii nyingine imetokea kule China ambapo mwanamke mmoja amejikuta akijifungua njiani bila kujua wakati anakwenda hospitali baada ya kusikia uchungu.

Qi aliongozana na mumewe Li wakitumia usafiri wa pikipiki kwenda hospitali ya Chenguang Nongchang kwa ajili ya kujifungua lakini kwa bahati mbaya mama huyo alijifungua njiani bila kutambua na mtoto kubakia barabarani ikiwa ni maili mbili kabla ya kufika hospitalini hapo.

Baada ya kufika hospitali na madaktari kumcheki walikuta tayari mtoto ametoka huku mama huyo akitokwa damu na baada ya kufanya uchunguzi iligundulika mama huyo amejifungua njiani akiwa njiani bila kujua na mtoto wake kuokolewa na watu wengine.

Mama huyo akiongozana na madaktari walirudi kuangalia ni wapi mtoto huyo amedondoka na kumkuta akiwa amezungukwa na watu bila kuwa jeraha lolote na kumkimbiza hospitali ili kufanyiwa uchunguzi wa kina juu ya afya yake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post