BAADA YA KUNUSURIKA KUPINDULIWA_RAIS NKURUNZIZA AFUNGUKA,ADAI "ATALIPIZA KISASI KWA WABAYA WAKE"

 
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amewapongeza wanajeshi wazalendo waliozuia mapinduzi na kurejesha hali ya usalama na utawala huru mjini Bujumbura.

Meja jenerali Godefroid Niyombare,aliyetangaza ''mapinduzi''
Rais Nkurunziza amewataka waburundi wazalendo kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi utakaofanyika mwezi juni.

Rais huyo alikuwa Mjini Dar es Salaam Tanzania siku ya Jumatano kuhudhuria mkutano wa viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki kundi la wanajeshi waasi walipotangaza ''Mapinduzi'' dhidi ya serikali yake.
Rais Nkurunziza
Viongozi watatu miongoni mwa makamanda6 wa jeshi waliounga mkono tangazo hilo la ''mapinduzi'' ilikupinga muhula wa tatu wa rais huyo tayari wamekamatwa.

Kufikia sasa watu 105,000 wameripotiwa kutorokea mataifa jirani kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa.

Baada ya kurejea kutoka Tanzania rais Nkurunzinza alielekea Kaskazini mwa Bujumbura eneo alikotokea kabla ya kurejea katika kasri la rais lililoko katika mji mkuu wa Bujumbura.

Katika taarifa iliyochapishwa mtandaoni rais Nkurunzinza alisema kuwa ''
Kuna amani na utangamano katika asilimia kubwa ya Burundi na hata katika mji mkuu wa Bujumbura ila tu watu wachache waasi ndio waliokuwa na hamu ya kuvuja damu''

''Jeshi la taifa lilionesha ukomavu wake lilipokabiliana na wasaliti hao''

''Ningependa kuwahimiza waburundi wazalendo walinde kwa dhati amani iliyoko sasa kwani ndio ngao na msingi wa demkrasia iliyoko Burundi''

''Shari msingi wa demokrasia yetu changa ilindwe isiyeyuke''
Nkurunziza aliahidi kulipiza kisasi dhidi ya ''yeyote aliyejaribu kuwasha moto wa uhasama baina ya waburundi''

Rais Nkurunzinza aliwasili mjini Bujumbura Ijumaa akiwa ameambatana na maelfu ya wafuasi wake.
Wengi wao wafuasi wa chama chake ambao walimshangilia kwa kurejea kwake huko .

Mwandishi wa BBC aliyeko huko Ruth Nesoba anasema japo asilimia kubwa ya mji huo ulikuwa na amani, katika sehemu zingine kulikuwa na waandamanaji walioweka vizuizi barabrani wakipinga kuwania kwake kwa muhula wa tatu.

Polisi wa kupambana na ghasia walikuwa wakikabiliana nao kwa kuwafyatulia mabomu ya kutoa machozi.
Miongoni mwa makamanda waliokamatwa kwa kuchochea uasi ni pamoja na waziri wa zamani wa ulinzi Cyrille Ndayirukiye.

Waziri wa sasa wa usalama Gabriel Nizigama aliiambia BBC kuwa maafisa wawili wakuu katika idara ya polisi pia walikamatwa pamoja na wadogo wao takriban 12 waliokuwa wakiwalinda.

Wawili hao walikamatwa baada ya ufyatulianaji wa risasi nje ya jumba walimokuwa.

Kiongozi wa uasi huo meja jenerali Godefroid Niyombare,aliyetangaza ''mapinduzi'' hayo siku ya jumatano hajakamatwa japo alinukuliwa na shirika la habari la AFP akisema kuwa atajisalimisha.

''Nitajisalimisha kwa utawala, natumai hawataniua'' alisema meja jenerali Niyombare.
Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post