UNAKUMBUKA ISHU YA WANAWAKE KUPIMWA BIKRA ILI KUJIUNGA NA JESHI? BASI KINACHOENDELEA SASA KIKO HAPA

Indonesia imeshauriwa ikomeshe sheria inayowalazimu wanawake kuthibitisha ni mabikira kabla ya kujiunga na jeshi la taifa.


Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wameihimiza serikali ya Indonesia kukomesha kipengee kimoja cha kubainisha iwapo mwanamke ni bikira au la kabla ya kujiunga na jeshi la taifa.
Wanaharakati hao wanasema kuwa ni tukio linalodhalilisha wanawake hao kwa misingi ya kijinsia.

Shirika la afya duniani WHO limepinga sheria hiyo likisema halina misingi yeyote kiafya.

Aidha shirika la Human Rights Watch (HRW) inaongezea kusema kwamba mtu kuwa au kutokuwa bikira hakuathiri utenda kazi na uwajibikaji wa mwanamke kazini.

Lakini je nini kinachoendelea Indonesia?
Wanaharakati hao wanasema kuwa wengi wa makurutu ambao huwa ni wasichana waliohitimu shule ya upili wenye umri kati ya miaka 18-20 hulazimika kukaguliwa sehemu zao za uzazi ilikuthibitisha wangali ''wasafi na hivyo wazalendo''.

Kulingana na shirika la kutetea haki za kibinadamu, sasa hata wachumba wa wanajeshi wao hawasazwi.

''wachumba wa wanamaji, wanajeshi wa angani na wanajeshi wa ardhini sasa wanalazimika kupimwa ubikira kabla ya kuruhusiwa kuolewa na maafisa''asema mwanaharakati mmoja.

Mwezi Februari maafisa wa jimbo la Jember ,Java Mashariki waliharamisha kujaribiwa kwa wasichana kabla ya kuhitimu shule za upili.

Je kipimo hicho kinafanywaje ?
Kulingana na mtafiti mmoja Andreas Harsono kipimo hicho kijulikanacho kama "two-finger test", kinatumika na madaktari kubaini iwapo mwanamke ni bikira au la.

Daktari anapaswa kung'amua iwapo mwanamke huyo ameshiriki tendo la ndoa au la.

''Daktari anatumbukiza vidole viwili ndani ya uke na kimoja katika tupu ya nyuma ''alisema mama mmoja mke wa mwanajeshi ambaye pia ni askari.

Bwana Harsono aliwahoji wanawake 11 wengi wao wake wa wanajeshi na wengine maafisa kivyao.
Hadi sasa haijabainika faida ya kipimo hicho ambacho kinalaumiwa kuwa kinawadhalilisha wanawake.

Amiri mkuu wa jeshi la Indonesia Meja Jenerali Fuad Basya,amesema kuwa kipimo hicho ni nguzo ya uzalendo na swala muhimu katika usalama wa taifa.

''Haiwezekani iwapo mtu ni msherati si muaminifu kwa mumewe apewe jukumu la kulinda usalama wa taifa''alisema Jenerali Fuad.

Kama mtu anapania kulinda mipaka ya taifa na pia usalama wa mamilioni ya watu ilihali ameshasaliti nafsi ya mumewe basi mtu kama huyo hapaswi kupewa jukumu la kulinda taifa''

''kama mwanamke si bikira iwe amegonjeka ama amejamiani hafai kuwa askari Hafai kuhudumu katika jeshi la Indonesia '' Jenerali Fuad alianukuliwa na vyombo vya habari.

Hata hivyo majibu yake yalitofautiana na ya mke mmoja wa mwanajeshi ambaye mwenyewe ni askari aliyesema kuwa walipewa sababu tofauti ya kipimo hicho.

''Wajua jeshi la Indonesia linataka wanajeshi wenye siha nzuri kwa hivyo wanalazimika kutumia mbinu kama hizo kupunguza gharama za matibabu ''

''Wanajeshi wetu wanasafiri kila baada ya muda na hivyo wanastahili kuamini kuwa wanawake wao na hata waume pia ni waaminifu''

Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post