JINSI MOTO ULIVYOTEKETEZA GHALA LA KUHIFADHIA BIDHAA MBALIMBALI ZA KAMPUNI YA KAHAMA OIL MILLS YA MJINI KAHAMA


Muonekano wa ghala hilo lilivyoathiriwa na moto huo.

Bidhaa mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 3 zimeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo, katika ghala la kuhifadhia bidhaa za kampuni ya Kahama oil mills wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Akizungumza na wandishi wa Habari ofisini kwake meneja mkuu wa kampuni hiyo William Matonange, amesema chanzo cha tukio hilo inadaiwa kuwa ni kuripuka kwa baadhi ya bidhaaa zenye asili ya kuripuka zilizokuwa zimehifadhiwa katika ghala hilo.


Aidha meneja huyo amesema bidhaa zilizoteketea zilikuwa na thamani ya zaidi ya shilling bilioni 3 huku jengo likiwa lenye thamani zaidi ya shilingi bilioni 1. 

Akifafanua zaidi amesema moto huo unasadikiwa ulianza usiku wa manane ambapo uligundulika majira ya saa tisa usiku ndipo walipotoa taarifa kwa jeshi la polisi kitengo cha zimamoto ambao walifika na kuanza kuuzima ambao ulidumu kwa masaa sita.


Hata hivyo Matonange amelipongeza jeshi la polisi mkoani Shinyanga kwa juhudi za kuimarisha ulinzi katika zoezi la kuzima moto kutokana na wananchi walikuwa na lengo la kuvamia kiwanda hicho kwa ajili ya kwenda kupora mali wakati jeshi la zimamoto likiendelea na zoezi la kuuzima moto huo.

Kwa upande wake kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga Justus Kamugisha  amesema uchunguzi unaendelea hivyo taarifa zaidi zitatolewa baada ya wataalam kutoka kitengo cha bima kufanya uchunguzi wao.Na Emmanuel Mlelekwa  - Kahama

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post