BASI LA UNIQUE EXPRESS LAGONGANA NA LORI LA COCACOLA SAMUYE SHINYANGA,WATU 10 WAFARIKI,MAJERUHI 50
Wednesday, April 22, 2015
Miili ya abiria ikiwa imenasa katika basi la Unique
Ajali za barabarani zimeendelea kujitokeza ambapo leo majira
ya saa tisa kasorobo alasiri Watu 10 wamefariki dunia na wengine 50 kujeruhiwa
baada ya basi la Kampuni ya Unique Express lenye namba za usajili T148 BKK kugongana na lori aina ya scania lenye namba za usajili T207 BSA na tela lenye
namba za usajili T635 AJT mali ya kampuni ya Coca Cola katika barabara ya Tinde
Shinyanga eneo la kijiji cha Ibingo kata ya Samuye wilaya ya Shinyanga mkoani
Shinyanga.
Mashuhuda wa tukio wameiambia Malunde1 blog kuwa dereva wa
lori alikuwa anaendesha gari akiwa katikati ya barabara huku dereva wa basi akiwa
katika mwendo kasi hali ambayo katika kukwepa basi hilo aligonga tela la lori kisha
kupinduka.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha
aliyeko eneo la tukio amesema watu 10 wamepoteza maisha katika ajali hiyo
kati yao 9 walifariki dunia papo hapo huku majeruhi 50 wakiwemo wanawake 13,wanaume 36 na mtoto mmoja
wa kiume wanapata matibabu katika
hospitali ya mkoa wa Shinyanga.
Social Plugin