Mtu mmoja ameripotiwa kufariki na wengine 240 kujeruhiwa baada ya treni mbili kugongana katika mji wa Johannesburg nchini Afrika Kusini.
Afisa mmoja wa usalama amesema kuwa ajali hiyo imetokana na msongamano wa wa misafara ya asubuhi.
Afisa huyo ameongeza kwamba treni moja iliyokuwa imeegeshwa katika kituo
cha Denver kilichoko kusini mwa mji wa Johannesburg, iligongwa na treni nyingine iliyowasili kutoka jijini Pretoria.
Mlinzi mmoja wa eneo hilo alifariki katika ajali hiyo huku watu wengine 240 wakijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.