Heeh!! KANISA HILI WANASALI UKIWA UCHI WA MNYAMA KABISAA,WANAWAKE NA WANAUME

Praying-hands-with-bible

Malalamiko yalikuwa mengi tangu kufunguliwa kwa kanisa hilo la Healing Ministry katika Kaunti ya  Machakos, Kenya.. wanawake wanaingia kwenye migogoro na wanaume zao kisa ibada, wakati mwingine walikua wanaenda kulala huko huko.

Hii kitu ikaleta migogoro mingi kwenye baadhi ya familia, baadae kukawa na malalamiko kwamba wanawake wanaosali kwenye Kanisa hilo wanasali wakiwa wamevua nguo zote.. 

Watu wa eneo hilo wamevamia kanisani hapo usiku, wakakuta wanawake wakiwa wanasaliwa huku wamevua nguo zote.. Kasisi akajitetea kwamba alikuwa akiwafanyia ibada maalum.

Mwenyekiti wa muungano wa wafanyabiashara eneo hilo Duncan Mutua amesema; “Tulivamia kanisa hilo na kumfumania Kasisi akiwamwagilia wanawake maji wakiwa uchi wa mnyama alijitetea akisema alikuwa akiwafanyia maombi spesheli,”.

Amesema wasiwasi kuhusu shughuli za Kanisa hilo uliongezeka baada ya wanawake wa eneo hilo kutumia muda wao mwingi Kanisani na hata kuwaacha waume wao usiku na kwenda kwenye ibada za mkesha.

TFCHURCH2404
Hilo ndiyo kanisa ambalo limetuhumiwa kufanya ibada za wanawake wakiwa hawana nguo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post