SHEIKH WA WILAYA AFARIKI GHAFLA MAKABURINI BAADA YA KUSWALISHA SWALA YA MAZISHI YA MAMA

Tunataka Tukutumie Habari zetu mara tu Tunapoziweka Mtandaoni,Bonyeza Hapa

Sheikh mkuu wa wilaya ya Mbeya mjini, Bakari Mketo amefariki dunia ghafla makaburini mara baada ya kuswalisha swala ya mazishi katika makaburi ya Nonde jijini na mkoani Mbeya jioni ya jana.

Tukio hilo limetokea juzi jioni.


Sheikh huyo maarufu kwa jina la Mketo mkazi wa Nonde anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 50-60 amekutwa na mauti katika eneo la makaburi hayo ya Nonde mara tu baada ya kumaliza kutoa mawaidha kwa watu waliojumuika kumzika mama aliyefariki katika hospitali ya rufaa Mbeya juzi na msiba wake kuwekwa nyumbani kwake Sokomatola katikati ya jiji la Mbeya.

Inaelezwa kuwa  shekhe Mketo alitoa huduma zote tangu mwanzo wa msiba mpaka alipokutwa na mauti.


Kwa mujibu wa mashuhuda ya kifo cha sheikh Mketo waliokuwa katika makaburi hayo, wamesema kuwa marehemu Mketo hakuwa na dalili zozote za ugonjwa na wala hakulalamika kujisikia vibaya kabla ya kukutwa na mauti hayo.


Aidha mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa wakati akitoa mawaidha makaburini hapo sheikh Mketo alisisitiza sana juu ya vijana kujifunza na kuifuata vema elimu ya kiislamu na kuishika vilivyo kwani kifo hakina taarifa na akatolea mfano kuwa hata yeye anaweza kukutwa na mauti papo hapo katika eneo la makaburi na akalisisitiza hili zaidi ya mara tatu ndipo muda mfupi baadaye akadondoka na kupoteza maisha yake.

Via>>Fichuotz.com

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527