Ushirikina!! VIJANA WAWILI MBARONI KWA KUKUTWA NA KIDOLE CHA BINADAMU,ETI UKIWA NA KIDOLE HICHO UNAPATA MALI KIBAO

Wakazi wawili wa kijiji cha Mazombe, mkoani Iringa wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa tuhuma za kukutwa na kidole cha binadamu kwa kile kinachodaiwa kuwa kutokana na imani za kishirikina.
 
Kaimu Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoani Iringa, Wankyo Nyigesa alisema tukio hilo limetokea juzi na kuwataja watuhumiwa hao kuwa ni Gibson Kasenegala (29) na Benson Mlasu (23).
 
Alisema watuhumiwa hao kwa pamoja walikuwa wakimiliki kidole hicho ambacho hakijulikani  kuwa ni cha nani, ambapo inasemekana kwamba wakiwa na kidole hicho kinaweza kuwasaidia kupata mali.
 
“Tumewatia mbaroni na uchunguzi wetu unaendelea ili tujue nani alikatwa kidole, au kama kuna mtu aliuawa kisha kidole chake kikachukuliwa,” alisema Nyigesa.
 
Alisema watuhumiwa hao kwa pamoja wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya uchunguzi huo kukamilika.
 Na Frank Kibiki-Iringa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post