MWALIMU AKATWA KIGANJA CHA MKONO KWA PANGA NA MWANAYE HUKO MBEYA

 
Mwalimu mmoja mkazi wa eneo la Iwindi Mbeya Vijijini mkoani Mbeya, amekatwa kiganja  cha mkono wake na mtoto wake wa kumzaa.

Tukio hilo limetokea jana asubuhi kijijini huko, baada ya kutokea taflani kwenye familia hiyo.

Kukatika kwa kiganja kwa Mwalimu huyo, kumeelezwa kuwa kulitokana na kitendo chake cha kukinga upanga uliokuwa ukimwendea katika mwili wake.

Chanzo halisi cha ugomvi wa familia hiyo bado hakijajulikana ingawa kuna taarifa ambazo siyo rasmi kuwa kuna mtafaruku wa muda mrefu ndani ya familia hiyo jambo ambalo limeelezwa kuwa baadhi ya ndugu wamefurahia Mwalimu huyo kupatwa na tafrani hiyo.
via>>Kalulunga blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post