Duh!!!! KIJANA ABAKA KIKONGWE KICHAKANI,AFUNGWA MIAKA 30 JELA HUKO KATAVI

 
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imemuhukumu John Joseph (30) kwenda jela miaka 30 baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanamke mzee wa miaka 65.

 
Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda, Chiganga Ntengwa baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.
 
Awali katika kesi hiyo Mwendesha Mashitaka, Godfrey Luzabila alidai mahakamani hapo kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Agosti 18 mwaka jana saa 12 jioni katika Kijiji cha Ifukutwa, Tarafa ya Kabungu wilayani Mpanda ambako mshitakiwa alikwenda kufanya kibarua cha kutengeneza barabara.
 
Alidaiwa kwamba siku ya tukio alimwona mwanamke huyo akipita barabarani ndipo mshitakiwa alimfuata na kumvutia kichakani pembeni ya barabara iliyokuwa ikijengwa.
 
Mwendesha mashitaka huyo aliiambia mahakama kuwa mshitakiwa baada ya kumvuta kikongwe huyo porini alimlazimisha wafanye ngono kitendo ambacho mwanamke huyo alikikataa.
 
Ilielezwa mahakamani hapo kwamba mbakwaji alimsihi mshitakiwa asifanye hivyo, maombi ambayo hakukubaliana nayo ndipo alipomshika na kumvua nguo kwa nguvu kisha kuanza kumbaka wakati mwanamke huyo akipiga kelele za kuomba msaada.
 
Mwendesha mashitaka alidai mahakamani hapo kwamba kelele za mbakwaji zilisaidia kupata msaada kutoka kwa watu watatu waliokuwa wakipita eneo hilo ambao walikwenda na kumwona mshitakiwa akimbaka mwanamke huyo kabla ya kukimbilia kichakani.
 
Hakimu Ntengwa akisoma hukumu hiyo alisema kutokana na ushahidi wa watu watatu uliotolewa na upande wa jamhuri pamoja na taarifa ya daktari akithibitisha ubakaji uliosababisha sehemu za siri za mwanamke huyo kuharibika, mahakama imemtia hatiani mshitakiwa huyo na kumhukumu kwenda jela miaka 30.
 
Via>>Tanzania Daima 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post