Shinyanga Kumekucha!!! PSPF WADHAMIRIA KULETA MAPINDUZI,FUATILIA TUKIO ZIMA LA ZIARA YAO HAPA

Ziara ndiyo Inaanza:Ni katika siku ya pili (Jana) ya ziara ya Afisa mfawidhi PSPF mkoa wa Shinyanga Erick Chanimbaga (katikati),akiwa ameambatana na mjumbe wa bodi ya PSPF Clement Mswanyama(wa kwanza kushoto),mkoani Shinyanga inayolenga kutoa elimu kuhusu mpango wa uchangiaji wa hiari ulioanzishwa na PSPF .Hapa ni katika kiwanda cha pamba cha Afrishian kilichopo eneo la Ibadakuli mjini Shinyanga wa kwanza kulia ni meneja uhusiano wa kiwanda hicho Ally Habshy akisikiliza maelezo  kutoka kwa Mswanyama kuhusu namna mpango wa uchangiaji hiari utakavyonufaisha wafanyakazi wake


Kushoto ni  Afisa mfawidhi PSPF mkoa wa Shinyanga Erick Chanimbaga akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha Afrishian juu ya mpango wa uchangiaji wa hiari ambapo afisa huyo alisema ukijiunga na mfuko huo unaweza kuchangia kuanzia shilingi elfu kumi na akasisitiza hakuna kima cha juu cha uchangiaji.
Ziara inaendelea:Hapa ni ndani ya ofisi ya mkurugenzi wa Jambo Group of Company Ltd, Suleiman  Khamis Salum(katikati) baada ya afisa mfawidhi PSPF mkoa wa Shinyanga Erick Chanimbaga kufika katika eneo hilo kwa ajili ya kuzungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo.Suleiman  Khamis Salum aliwaasa wafanyakazi wake kutumia fursa hiyo kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari ambao una faida kutokana na kwamba uchangiaji wake ni rahisi pia ni nzuri kwa kuweka akiba ya uzeeni


Afisa mfawidhi PSPF mkoa wa Shinyanga Erick Chanimbaga akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha maji katika kampuni ya Jambo ambapo alisema mpango huo umeanzishwa na PSPF kwa ajili ya kupanua wigo wa uanachama kwa kuandikisha wananchi waliojiajiri au kuajiriwa katika sekta rasmi na isiyo rasmi ambapo miongoni mwa mafao yanatolewa na mfuko huo kuwa ni pamoja na fao la elimu,fao la ujasiriamali,fao la uzeeni,fao la kifo,fao la kujitoa na fao la ugonjwa ama ulemavu


Baadhi ya Wafanyakazi wa kampuni ya Jambo wakimsikiliza afisa huyo kutoka PSPF ambaye aliwasisitiza kujiunga na mfuko wa hifadhi ya jamii ambapo alisema kuna namna tatu za kuchangia kama vile kwa wiki,mwezi au msimu kutegemea na upatikanaji wa kipato cha ziada kwa ajili ya akiba
Afisa mfawidhi PSPF mkoa wa Shinyanga Erick Chanimbaga alisisitiza kwamba hata kama mwanachama anachangia mpango wa lazima (main scheme) wa mfuko mwingine lakini bado anaweza kuwa mwanachama wa mfuko wa hiari wa PSPF.

 Wa kwanza ni Marco Maduhu mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe akiandika mawili matatu yaliyokuwa yanaendelea......
Ziara inaendelea: Hapa ni ndani ya ofisi ya meneja wa kampuni ya Fresho Investment(kiwanda cha pamba) bwana Ndalahwa(kwa kwanza kushoto) baada ya afisa mfawidhi PSPF mkoa wa Shinyanga Erick Chanimbaga(hayuko pichani) kuwasili katika kiwanda hicho kwa ajili ya kutoa elimu kwa wafanyakazi kuhusu mpango wa uchangiaji hiari


Kushoto ni afisa biashara sekretariati ya mkoa wa Shinyanga Ibrahim Masalamado aliyekuwa ameambatana na afisa huyo wa PSPF akisisitiza jambo ndani ya ofisi ya meneja wa Fresho Investment company limited 
Ziara Inaendelea: Hapa ni katika Shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo(SIDO) mkoa wa Shinyanga,kulia ni  afisa uendelezaji wa biashara wa SIDO mkoa wa Shinyanga bi Bahati Mkopi,kulia kushoto ni afisa mfawidhi PSPF mkoa wa Shinyanga Erick Chanimbaga akizungumza na vikundi mbalimbali vya wajasiriamali,ambapo aliwaasa kutumia fursa ya mpango wa uchangiaji hiari kwani unawapa nafasi ya kuchangia kidogo kidogo kwa manufaa yao binafsi 
Wajasiriamali mbalimbali(wakulima,mama lishe,wadau wa ngozi,mafundi n.k) wakimsikiliza afisa huyo kutoka PSPF ambapo alisema mpango wa uchangiaji wa hiari unalenga kuwafikia watu wote bila kusahau wenye kupato cha chini,ambapo mwanachama atakuwa anapata riba kila baada ya miezi 6
Afisa mfawidhi PSPF mkoa wa Shinyanga Erick Chanimbaga akiendelea kuwafunda wajasiriamali hao ambapo alisema mwanachama anaweza kuwasilisha michango yake moja kwa moja kupitia akaunti ya benki au kwa wakala wa malipo wa M-PESA,TIGO PESA NA AIRTEL MONEY,ambapo kiwango cha uchangiaji ni kuanzia shilingi elfu kumi au zaidi na kwamba ofisi za PSPF katika mkoa wa Shinyanga zipo kwenye jengo la Benki ya posta ghorofa ya pili mjini Shinyanga.
Ziara Inaendelea:Hapa ni katika viwanja wa Mazingira senta mjini Shinyanga ambapo afisa huyo kutoka PSPF Erick Chanimbaga(aliyesimama) alikutana na waendesha pikipiki(Boda boda) pamoja na waendesha taxi wa mjini Shinyanga na kutoa elimu kuhusu mpango wa uchangiaji wa hiari ulioanzishwa na mfuko
wa pensheni wa PSPF.Wa pili kutoka kushoto ni mwenyekiti wa chama cha waendesha pikipiki  katika manispaa ya Shinyanga,bwana Mohamed Juma,wa kwanza kulia ni makamu mwenyekiti wa waendesha taxi katika manispaa ya Shinyanga bwana Joseph Tasia


Aliyesimama ni mwendesha bodaboda Marcel Bukwimba akiuliza swali kwa afisa mfawidhi PSPF
Waendesha bodaboda na taxi wakifuatilia kilichokuwa kinajiri katika viwanja vya Mazingira senta jana mjini Shinyanga wakati wa ziara ya afisa mfawidhi PSPF

<<BOFYA HAPA KUJUA KILICHOJIRI SIKU YA KWANZA YA ZIARA YA PSPF MKOANI SHINYANGA>>

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post