Mauaji Shinyanga!! MWANAMKE AUAWA KWA KUCHARANGWA MAPANGA,KIJANA APIGWA MAWE KISHA KUCHOMWA MOTO

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangalla
Watu wawili wamefariki dunia mkoani Shinyanga katika matukio mawili tofauti likiwemo la mwanamke mmoja kuuawa kwa kucharangwa mapanga akiwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana na tukio la pili likiwa ni kijana kuuawa kwa kupigwa mawe baada ya kutuhumiwa kuiba baiskeli.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangalla amesema tukio la kwanza limetokea Aprili 3 mwaka huu,saa kumi jioni, ambapo mwanamme mmoja asiyejulikana kwa jina,kabila wala makazi yake mwenye umri kati ya miaka 25 hadi 30 aliuawa kwa kupigwa mawe kisha mwili wake kuchomwa moto na wananchi waliojichukulia sheria mkononi katika kijiji cha Usanda wilaya ya Shinyanga vijijini.

Amesema wananchi hao walifanya mauaji hayo baada ya kumtuhumu kijana huyo kuiba baiskeli aina ya Sancos  Sindelela ambayo haijajulikana thamani yake wala mmiliki wake.

Kamanda Mangalla amesema baada ya wananchi hao kufanya mauaji hayo wananchi hao waliondoka na kutokomea na baiskeli hiyo kusikojulikana. 

Kamanda Mangalla amesema tukio la pili  limetokea hilo limetokea Aprili 3 mwaka huu saa mbili asubuhi katika kijiji cha Zumve,kata ya Nindo,wilaya ya Shinyanga vijijini ambapo mwanamke mmoja  ameuawa baada ya kukatwa kwa panga kichwani,paji la uso na shingoni na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake.

Amemtaja mwanamke aliyeuawa kuwa ni Sophia Malandu mwenye umri kati ya miaka 50 hadi 55.

Kamanda Mangalla amewaasa wananchi kutojichukulia sheria mkononi na kuwataka kutoa ushirikiano ili kuwabaini na kuwakamata wahusika wa mauaji hayo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments