Uchawi!!!!! AFISA WA WIZARA YA ELIMU APEWA JENEZA LIKIWA NA MZOGA WA PAKA NJE YA NYUMBA YAKE

Familia ya Bwana Oganda inasema kuwa sio mara ya kwanza kwa kisa kama hiki kuikumba
Familia ya afisa mmoja wa Elimu nchini Kenya imepigwa na butwaa baada ya kupata jeneza dogo likiwa limewekwa kwenye mlango wao mjini Kisumu Magharibi mwa Kenya.


Kwa mujibu wa taarifa ya gazeti la Taifa Leo, familia ya Afisa huyo Elias Oganda, mwenye umri wa miaka 56, ilipata jeneza hilo dogo likiwa na mzoga wa Paka nje ya mlango wao na sasa inaishi kwa hofu kubwa.


Afisa huyo anayefanya kazi katika wizara ya elimu, alisema kuwa hii ni mara ya nne katika miezi sita kupata jeneza kama hilo nyumbani kwake.

Polisi walifungua jeneza hilo na kupata mzoga wa Paka ndani yake. Walishuku kuwa Paka huyo alinyongwa na kuwekwa ndani ya jeneza hilo kwani hapakuwa na dalili yoyote ya damu.

Afisa mkuu wa polisi katika eneo hilo amesema kuwa hili sio tukio la kwanza kushuhudiwa katika eneo hilo.

Bwana Oganda naye alisema kuwa jeneza hilo liligunduliwa na mkewe Joyce Oganda, mwenye umri wa miaka 50, usiku wa manane alipotoka nje kujisaidia.

''Nia ya mtu aliyefanya kitendo hicho haijulikani, mimi sijawahi kuhusika na mzozo wa ardhi , familia yangu haijawahi kupata ,utulivu kwa mwaka mmoja uliopita kwani nimekuwa nikifanyiwa uchawi mara kwa mara.'',alisema Oganda.

''Hii ni ardhi ya babaangu na sielewi kwa nini watu wanataka kunitishia maisha kwa kutumia uchawi.''

Wakazi wa eneo hilo walifika kwa wingi katika nyumba ya bwana Oganda kushuhudia mganga wa jadi aliyeletwa katika nyumba hiyo kutoka Sirari mpakani mwa Kenya na Tanzania kujaribu kujua ni nani aliyehusika na kitendo hicho.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post