Sakata la Diwani wa CCM kukamatwa na Kadi FEKI za CHADEMA huko Geita !!!! BAVICHA WATOA TAMKO FUATILIA HAPA


Sakata la diwani wa CCM viti maalumu Bi Zaituni Fundikira  katika kata ya Kalangala wilayani Geita mkoani Geita kukamatwa na kadi 23 feki za chama cha demokrasia na maendeleo Chadema kwenye mkoba ndani ya nyumba anayoishi zikiwa na sahihi ya kugushi ya mwanyekiti wa CHADEMA taifa Freeman Mbowe, limechukua sura mpya baada ya mwenyekiti wa baraza la  vijana Chadema (BAVICHA) kata ya kalangalala wilayani humo  Deogatias Shinyanga  kukemea vikali na kulaani kitendo cha diwani huyo.


Akizungumza jana kwenye kikao kilichofanyika kwenye viwanja vya Ihayabuyaga mjini Geita kwa lengo la  kutoa tamko kuhusu diwani huyo amesema kitendo  alichofanya diwani huyo ni cha kihuni na cha kudharirisha chama chao hivyo wanalaani na kukemea kitendo hicho.

Shinyanga amewataka wananchi wa mkoa wa Geita kuachana na siasa  za propaganda uchwara za wana ccm kwani hawana jipya na wamekuwa wakitumia kadi zao za kugushi na kwenda nazo kwenye mikuatano yao na kuzitoa wakidai wamepata wanachama wapya huku ukiwa ni uongo mkubwa.

 Ameongeza kuwa  japokuwa wamefungua kesi polisi watahakikisha kesi inafika mahakamani na kuhakikisha yeye kama mwenyekiti wanashinda ili hilo liwe fundisho  kwa viongozi wengine wanaofikiria kufanya vitendo hivyo vya kugushi sahihi za viongozi.

wananchi waliongea na mwadishi wa habari hii wamelaani vikali kitendo cha diwani huyo kukamatwa na kadi huku akidai yeye amepewa na machokola kitendo ambacho kilivuta sana hisia za wakazi wa Geita wakiwemo wakereketwa wa Chadema.

Wiki iliyopita diwani wa CCM wa viti maalumu  Bi, Zaituni Fundikira wa kata ya Kalangalala alikamatwa na kadi 23 za chama cha demokrasia  na maendeleo zilizokutwa kwenye mkoba wake huku yeye akidai amepewa  na machokoraa wanaoishi kwenye pagale(nyumba ambayo haijaisha kujengwa.

Na Valence Robert -Geita.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post