Ukatili!!! BABA AUA MTOTO WAKE KWA KUMZIBA PUA NA MDOMO HUKO NJOMBE


kamanda wa polisi mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani


Jeshi la polisi mkoani Njombe linamshikilia Bw. Yusufu Sadick Mkalile (33) kwa tuhuma za kumuua mtoto wake wa kumzaaa mwenyewe kwa kumziba pua na mdomo

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari na Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani  imesema kuwa mtuhumiwa alitenda mauaji hayo Machi 16 mwaka huu majira ya saa 03:20 asubuhi, ambapo alimziba pua na mdomo mwanaye huyo aitwaye Udai Yusufu (8) hali iliyosababisha kukosa hewa na kufariki

Tukio hilo limetokea chumbani, nyumbani kwao mtaa wa Nazareth, kata ya Mjimwema tarafa ya Njombe Mjini wilaya ya Njombe, na hadi anafariki marehemu alikuwa akisoma darasa la pili katika shule ya Msingi Meta mkoani Mbeya

Mtuhumiwa wa mauaji hayo ambaye ni mkulima mkazi wa Stereo mkoani Mbeya amekamatwa na polisi na anaendelea kuhojiwa kuhusiana na mauaji hayo na chanzo bado hakijafahamika.
 Na Edwin Moshi- Njombe

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post