KUHUSU WATU WANNE KUUAWA KWA TUHUMA ZA WIZI WA WA NG'OMBE HUKO MWANZA

WATU wanne wameuawa mkoani Mwanza kwa tuhuma za wizi wa ng’ombe Katika eneo la Igwambiti kata ya Buhongwa Wilaya ya Nyamagana.
 
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Valentino Mlowola amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Jana majira ya  saa 11 alfajiri ambapo wananchi walipata taarifa ya kuwepo kwa  wizi wa ng’ombe katika kitongoji cha Mtende.
 
 Aidha, kamanda Mlowola amewataja waliofariki kuwa ni pamoja na  Ezekiel Lucas (27), Kusekwa Lucas (25), Masumbuko Kisinza (30) na Mafisi Mwita (26) ambao walishambuliwa na wananchi kwa  silaha za jadi kinyume cha sheria.
Hata hivyo, amesema tayari Jeshi la Polisi linawashikilia watu watatu kwa kukutwa  na silaha mbalimbali ambazo zimesadikiwa kutumika katika tukio hilo ,huku  uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post