Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeibuka mshindi wa jumla wa Tuzo za uandaaji bora wa vitabu vya hesabu katika Taasisi zote za Umma zinazotumia viwango vya kimataifa vya uandaaji wa hesabu katika sekta ya Umma (IPSASs) zilizotolewa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi Tanzania (NBAA) Novemba 26, 2026 Jijini Dar es Salaam.
Tuzo hiyo ambayo ni mara ya Tisa kwa TRA kushinda tangu kuanzishwa kwake imekabidhiwa kwa Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Juma Mwenda na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Mhe. Nsubili Joshua ambaye alisema ubora wa uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za fedha ni jukumu la uongozi wa taasisi na si idara za fedha pekee.
TRA pia imeibuka mshindi wa kwanza kwa mara ya 10 mfululizo wa Tuzo za uandaaji bora wa vitabu vya hesabu zinazotolewa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi Tanzania (NBAA) katika kundi la Taasisi za Wakala wa Serikali wanaotumia viwango vya kimataifa vya uandaaji wa hesabu katika sekta ya Umma (IPSASs).
Akizungumza baada ya kukabidhiwa Tuzo hizo Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Juma Mwenda amewataka Watanzania kuendelea kuiamini taasisi hiyo, akisema kodi wanazolipa zinasimamiwa kwa usalama na kutumika kwa manufaa ya umma.
Kushinda kwa Tuzo hizo kunaifanya TRA iwe na jumla ya Tuzo 2 kwa mwaka 2026 ambazo zinahusisha hesabu za mwaka 2025.



TAFUTA HABARI
Social Plugin