Tarehe 24 Novemba 2026, huko Ningbo, Zhejiang, China,roboti ya akili bandia ya kushona inayoitwa “Aini” ilianza kufanya kazi kwenye karakana ya uzalishaji wa kiwanda cha kaboni sifuri cha chapa ya nguo ya Taipingniao.
Roboti sita za Aini zilipangwa kwa mstari mmoja; zikitambua kitambaa, kuchukua vipande vilivyokatwa, kuvipanga sawa na kushona kwa mfululizo. Kwa siku zinaweza kutengeneza karibu jaketi 1,800 za manyoya.
Roboti hizi ni sehemu ya kundi la kwanza la “wafanyakazi wapya wa kushona” kutumiwa kwa kiwango kikubwa na makampuni ya nguo mkoani Zhejiang.
Roboti “Aini” zilibuniwa na kampuni moja ya teknolojia ya China. Kwa kutegemea teknolojia ya AI, zinaweza kurekebisha kwa wakati halisi kitambaa kinapokunjamana.
Kuanza kazi kwa “Aini” ni jaribio lingine la tasnia ya jadi ya mavazi ya Zhejiang kuelekea mageuzi ya uzalishaji wa akili bandia.

TAFUTA HABARI
Social Plugin