
Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akizungumza na wananchi wa kijiji cha Buchama.
**
Na Marco Maduhu, Stella Paul, SHINYANGA
Wananchi wa Kijiji cha Buchama Kata ya Tinde wilayani Shinyanga, ambao kijiji chao kimewekewa tenki kubwa la mradi wa maji ya Ziwa Victoria, lakini hawana maji, sasa wanatarajia kunufaika na huduma hiyo, baada ya Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad, kulisemea suala hilo Bungeni.
TAZAMA VIDEO👇👇
Hayo yamebainishwa Jana Septemba 30, 2026, katika mkutano wa hadhara wa Mbunge Azza, alipokuwa akizungumza na wananchi katika mkutano wa kuwashukuru pamoja na kusikiliza kero zao na kuzitolea majibu.
Azza amesema haiwezekani kijiji kama Buchama kuwa na tenki la mradi mkubwa wa maji ya Ziwa Victoria, ambayo yamesambazwa katika maeneo mengine, lakini kijiji hicho kisipate maji.
Amesema baada ya kuliona tatizo hilo, alilisemea Bungeni na maagizo yakatolewa kwa ajili ya utekelezaji zaidi.
“Maji ya Ziwa Victoria yatafika katika Kijiji hiki cha Buchama na vitawekwa vituo vya kuchotea maji. Na sasa ninavyozungumza na ninyi, Mkurugenzi wa SHUWASA yupo. Wizara ya Maji, kwa ajili ya jambo hilo, anasubiri apewe kibali ili atangaze kazi,” amesema Azza.
Naye Diwani wa Tinde, Jafari Kanolo, amemwomba Mbunge Azza kulivalia njuga suala hilo la maji ili wananchi wa Kijiji cha Buchama nao wanufaike.
Nao baadhi ya wananchi, akiwamo Paschali Richard, wamemshukuru Mbunge huyo kwa kuendelea kuwapigania katika kutatua changamoto mbalimbali, hasa tatizo la maji.
TAZAMA PICHA👇


































Social Plugin