Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

UONGOZI WA CATA WAIPONGEZA TANZANIA KWA MAANDALIZI NA USIMAMIZI WA MKUTANO WA 46

Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Wasimamizi wa Kodi wa Jumuiya ya Madola (CATA), Dkt. Esther A.P. Koisin, ameipongeza Tanzania kwa maandalizi na usimamizi mzuri wa Mkutano wa 46 wa CATA uliofanyika jijini Arusha.

Dkt. Koisin amesema maandalizi mazuri na ushirikiano uliotolewa umewezesha mkutano huo kufanyika kwa ufanisi, huku akitambua mchango wa Serikali na TRA katika kufanikisha mkutano huo.

Amesema Tanzania imeonesha uwezo wa kupokea na kusimamia mikutano ya kimataifa, na kuendelea kutoa mazingira mazuri ya kubadilishana uzoefu na kujenga ushirikiano katika masuala ya usimamizi wa kodi.

Aidha, amewashukuru viongozi, wajumbe na washiriki wote kwa ushiriki wao, akisema CATA itaendelea kuthamini ushirikiano na mchango wa Tanzania katika kuimarisha usimamizi wa mapato.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com