Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ROYAL SPLASH HOTEL YASAIDIA KOMPYUTA SHULE YA SEKONDARI CHALINZE





Na. ELISANTE KINDULU, CHALINZE.

SHULE  ya Sekondari Chalinze iliyopo Halmashauri ya Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani imepokea msaada wa kompyuta tano ambazo zimetolewa na Royal Splash Hotel na Splash lounge.

Akikabidhi msaada huo. Meneja wa Royal Splash Hotel na Splash Lounge bwana  Cosmas Michael amesema kuwa, kompyuta hizo ni sehemu ya mchango unaotokana na uwekezaji wa hotel hiyo katika eneo la Chalinze ili kuhakikisha wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo wanatumia zana za kisasa za kujifunzia ikiwamo kompyuta.

" Nikiwa mdau wa maendeleo, nimefurahi kutoa msaada huu ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaosoma kupitia zana za kisasa ikiwamo kompyuta ambazo ni uhitaji mkubwa katika shule hii", alisemma. 

Meneja huyo alisema  kuwa, hotel ya Royal Splash na Royal lounge ni sehemu ya uwekezaji unaofanyika katika Halmashauri ya Chalinze ili kutoa huduma Bora za malazi,Chakula, vinywaji, burudani, Kuogelea na Michezo mbalimbali kwa watoto.

Aliongeza kuwa, uwekezaji huo umesaidia kutoa jira Kwa vijana kutoka Chalinze na nje ya Chalinze ili kuhakikisha wanapunguza changamoto za upatikanaji wa ajira Ambapo jumla vijana 25 wamepata ajira kwenye eneo hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Chalinze Mwalimu Melkisedek Komba aliishukuru hotel hiyo kwa msaada huo na kuahidi kuzitumia kompyuta hizo kwa malengo yaliyokusudiwa.

" Kwa sasa elimu ipo kiganjani, shule nyingi zinatumia kompyuta Kwa ajili ya kuwafundishia watoto, hivyo basi msaada huu utasaidia kupunguza pengo la uhaba wa vitendea kazi ikiwamo kompyuta", aliongeza mkuu huyo wa shule. 

Royal Splasha Hotel na Splasha lounge zinahakikisha kuwa  asilimia 10 ya mapato, yanachangia kwenye miradi ya maendeleo na jamii ya Chalinze ambao kwa mawasiliano zaidi wanapatikana kwa  0790 129 503.














































































Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com