Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS RUTO AOMBOLEZA KIFO CHA RAFIKI YAKE 'CHIVAYO'



Rais wa Kenya, William Ruto, akiwa na mfanyabiashara wa Zimbabwe, Wicknell Chivayo (kushoto).

Rais wa Kenya, William Ruto, ameomboleza kifo cha mfanyabiashara wa Zimbabwe, Wicknell Chivayo, pamoja na mkewe, Lucy Muteke, waliofariki katika ajali ya helikopta nchini Zimbabwe.

Kupitia ukurasa wake wa X, Rais Ruto amesema amesikitishwa na kifo cha ghafla cha rafiki yake Chivayo, mkewe Lucy na watu wengine waliopoteza maisha katika ajali hiyo.

“Nimehuzunishwa sana na kifo cha ghafla na cha kusikitisha cha rafiki yangu Wicknell Chivayo pamoja na mkewe Lucy Muteke na watu wengine waliopoteza maisha katika ajali ya helikopta nchini Zimbabwe,” ameandika Ruto.

Rais Ruto amemuelezea Chivayo kama rafiki yake mpendwa ambaye ukarimu na upendo wake uliwagusa watu wengi, akisema atamkumbuka kwa urafiki wake, nguvu, ari na imani yake katika fursa na uwezo wa Bara la Afrika.

Aidha, Ruto ametoa pole kwa familia za wote waliopoteza maisha, Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa, wananchi wa Zimbabwe na wote wanaoomboleza msiba huo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, ajali hiyo ilitokea katika eneo la Marondera, Zimbabwe, majira ya saa 11 jioni kwa saa za Zimbabwe Septemba 30, 2026.

Polisi wamesema hakuna aliyenusurika katika ajali hiyo, huku moto uliotokea baada ya helikopta kuanguka ukifanya zoezi la kuwatambua wahanga kuwa gumu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com