Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, akizungumza wakati wa kufungua Kongamano la Mwaka la Tathmini ya Huduma za Habari na Mawasiliano Vijijini nchini Tanzania, lililoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini Tanzania (RUJAT), sambamba na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa chama hicho, jijini Dodoma, Oktoba 31, 2026. Picha na Kadama Malunde

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, akizungumza wakati wa kufungua Kongamano la Mwaka la Tathmini ya Huduma za Habari na Mawasiliano Vijijini nchini Tanzania, lililoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini Tanzania (RUJAT), sambamba na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa chama hicho, jijini Dodoma, Oktoba 31, 2026.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, akizungumza wakati wa kufungua Kongamano la Mwaka la Tathmini ya Huduma za Habari na Mawasiliano Vijijini nchini Tanzania, lililoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini Tanzania (RUJAT), sambamba na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa chama hicho, jijini Dodoma, Oktoba 31, 2026.
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Vijijini Tanzania (RUJAT), Neville Meena, akizungumza wakati wa Kongamano na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa chama hicho jijini Dodoma, Oktoba 31, 2026
Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Vijijini Tanzania (RUJAT), Prosper Kwigize, akizungumza wakati wa Kongamano na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa chama hicho jijini Dodoma, Oktoba 31, 2026
Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Vijijini Tanzania (RUJAT), Prosper Kwigize, akizungumza wakati wa Kongamano na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa chama hicho jijini Dodoma, Oktoba 31, 2026
Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya, ambaye pia ni mwandishi wa habari kitaaluma, akizungumza wakati wa Kongamano na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Waandishi wa Habari za Vijijini Tanzania (RUJAT), jijini Dodoma, Oktoba 31, 2026.
Na Dotto Kwilasa, Dodoma
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amewataka waandishi wa habari kurejesha ushawishi wao kwa wananchi kwa kuzingatia weledi, maadili na misingi ya taaluma.
Msigwa amesema ni muhimu kufanyika kwa utafiti kubaini sababu zinazowafanya wananchi kupunguza ufuatiliaji wa vyombo vya habari na kuelekeza imani yao katika makundi mengine yasiyo na jukumu la kitaaluma la kuhabarisha umma.
Ametoa wito huo Oktoba 31, 2026, jijini Dodoma, wakati wa Kongamano na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini Tanzania (RUJAT), ambapo pia ameahidi kutoa Sh milioni 10 kwa ajili ya kuimarisha shughuli za chama hicho.
Msigwa amesisitiza kuwa waandishi wa habari ni sauti ya wananchi na wanapaswa kusimamia maslahi ya jamii kwa ujumla bila kuongozwa na ajenda binafsi, huku akiwataka kuipa nafasi zaidi jamii za vijijini ambazo zinakosa uwakilishi wa kutosha katika maudhui ya vyombo vya habari.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa RUJAT, Neville Meena, amesema chama hicho kinalenga kuimarisha uandishi wa habari za vijijini kwa kuhakikisha waandishi wanachunguza namna miradi na matukio mbalimbali yanavyoathiri maisha ya wananchi badala ya kuripoti mikutano na matamko ya viongozi pekee.
Naye Katibu wa RUJAT, Prosper Kwigize, amesema chama hicho kimekua kutoka wanachama waanzilishi 20 mwaka 2020 hadi kufikia wanachama 120, huku kikiwa na maombi zaidi ya 60 kutoka kwa waandishi wanaotaka kujiunga.
Akizungumza katika kongamano hilo, Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya, amewataka wanahabari kuimarisha uchunguzi, ubunifu na ushindani wa kitaaluma, akisema baadhi ya waandishi wamekuwa wakitegemea taarifa za viongozi badala ya kufanya mahojiano na uchunguzi wa kina.















































































































































TAFUTA HABARI
Kamusi
Social Plugin